Showing posts with label KITAIFA. Show all posts
Showing posts with label KITAIFA. Show all posts

Friday, 12 January 2018

UVCCM: INAWEZEKANA TUSIFANYE KAMPENI 2020

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Kheri James amesema kuwa CCM haina sababu ya kufanya kampeni katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 badala yake kuna kila sababu ya kupita bila kupingwa kutokana na uimara wa CCM na serikali yake.
 Kheri ameyasema hayo wakati akizungumza na timu mbalimbali za kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kimandolu mkoani Arusha kutoka jumuiya za CCM.
 Kheri amesema serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na President Dr. John Pombe Magufuli imedhamiria kutatua kero zote zisizo rafiki kwa wananchi kwa utekelezaji wa mkataba wa wananchi na CCM kupitia ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020.
Amewafikishia wakazi wa Arusha salamu za JPM kuwa anahitaji ushindi wa kishindo wa zaidi ya kura 12,000 na hiyo itakuwa zawadi pekee kwake.
“Ndugu zangu sisi wana CCM tunaweza kujadiliana harusi itafungwa vipi na wapi, tunaweza tukajadiliana aina ya magari ya kununua lakini hatuwezi kuwa na mjadala wa namna yoyote ile kwenye utafutaji wa dola ni lazima CCM ishinde” -Kheri James
Share:

Monday, 13 November 2017

POLE YA MAKONDA KWA LULU YAZUA MTAFARUKU

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  leo ameposti kupitia account yake ya Instagram ujumbe wa kumpa moyo mwigizaji wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ baada ya Mahakama Kuu kumhukumu kwenda jela kwa miaka miwili  kwa kumuua mwigizaji Steven Kanumba.
Ujumbe huo ulikuwa na maneno: There is a room in every situation. Stay strong, Dady is coming! yakimaanisha kwamba kuna nafasi katika kila hali.  Endelea kujipa moyo, Baba anakuja!
Mkuu wa mkoa huyo hakufafanua wazi aliposema Baba, akimaanisha Baba Mungu au Baba yupi.
Share:

Sunday, 8 October 2017

PROF TIBAIJUKA ATOA CHANGAMOTO ANAZOPATA BAADA YA RUGEMALIRA KUWA MATATIZONI

Mbunge wa Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka amebainisha namna wanavyokabiliwa na changamoto katika uendeshaji wa Shule ya Wasichana ya Kajumulo Alexander iliyopo Bukoba baada ya mmoja wa wafadhili wa shule hiyo James Rugemalira kuwa matatizoni.
Prof. Tibaijuka amesema hakuanzisha shule kibiashara badala yake alijitoa kwa ajili ya kuwasaidia wasichana na kuwainua kielimu ndio maana anajitoa kwa kile alichonacho kuwasaidia watoto hao kwa kushirikiana na wafadhili wake huku akisema kuwa kwa sasa amebaki mwenyewe katika kuchangia baada ya mfadhili wake mkubwa James Rugemalira kushikiliwa na Polisi.
Share:

Monday, 2 October 2017

MANJI YAMKUTA TENA

Yusuf Manji
MAMALAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imezifunga ofisi za kampuni ya mfanyabiashara Yusufu Manji kutokana na kudaiwa Sh 12.2 bilioni.
Akizungumza leo Jumatatu jioni, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo amesema wamekuwa na mawasiliano na kampuni ya Farm Equpment ambayo inamilikiwa na Manji tangu Agosti 15 mwaka huu lakini kulikuwa hakuna mrejesho kuhusu deni hilo.
Kutokana na hilo amesema wamefunga ofisi zake kwa sababu kampuni hiyo inadaiwa kiasi cha Sh 12.2 bilioni lakini kampuni hiyo ina nafasi ya kuendelea kuwasiliana na TRA namna ya kulipa deni hilo.
Tukio hilo limetokea leo Jumatatu kati ya saa 4 hadi 7 wakati TRA na kampuni ya udalali ya Yono wakiambatana na polisi walipokwenda katika jengo hilo lililopo barabara ya Pugu, wilayani Temeke.
Baadhi ya mashuhuda wakiwamo walinzi kwa masharti ya kutotaja majina yao wameiambia Mwananchi kuwa ofisi zilizofungwa ni ya Manji na sehemu yake duka la kuuza pikipiki na matrekta.
Wamesema baada ya kufika watu waliingia moja kwa moja katika ofisi yake kisha kufanya majadiliano na wahusika yaliyodumu zaidi ya saa 2.
“Nadhani hawakufikiana mwafaka kwa sababu walivyotoka wakaamuru wafanyakazi wa ofisi hiyo kutoka nje kisha kuweka utepe wa rangi nyekundu na nyeupe,” amesema shuhuda huyo.
Hata hivyo, mashuhuda hao wamesema hawajui tatizo ni nini lakini waliwasikia maofisa wa TRA na kampuni hiyo ya udalali wakizungumza kuhusu kodi.
Share:

Sunday, 1 October 2017

ZITTO AIBUKIA BOT

Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe ameilalamikia benki kuu ya Tanzania kwa hatua yake ya kutokutoa taarifa za  hali ya uchumi za kila mwezi (Monthly Economic Review) kama inavyoelekezwa na sheria ya benki kuu ya mwaka 2006, Kupitia ukurasa wa Facebook wa Mbunge ameandika ujumbe huu...

"Miezi 4 Benki Kuu ( BoT ) imekalia Taarifa nyeti za Uchumi ( MER ). Kinafichwa nini?

Benki Kuu ya Tanzania inapaswa, Kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006 ikisomwa pamoja na kanuni zake, kutoa Taarifa ya kila Mwezi ya Mapitio ya Uchumi ( Monthly Economic Review). 

Tangu nianze kusoma Taarifa hizi nikiwa Chuo Kikuu hii ni Mara ya kwanza imepita miezi 4 MER haijachapishwa kwenye tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania. Mara ya mwisho imewekwa Taarifa ya Mwezi June inayoeleza mapitio ya mwezi Mei 2017. Taarifa hiyo ya mwisho ilionyesha kuwa mauzo yetu nje Kwa bidhaa za viwanda yameporomoka Kwa zaidi ya USD 700 milioni sawa na Bombadier mpya 21 Hivi.

Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano ambayo imejiondoa kwenye Mpango wa kuendesha Serikali Kwa Uwazi ( OGP ) na kujipa Sifa ya kufungia magazeti kuliko Awamu yeyote tangu tupate Uhuru Sasa imeamua kutunyima na Taarifa za kisheria kabisa kuhusu Uchumi.

Kwa kuchelewa huku, Taarifa itakayotoka lazima itakuwa ya kupikwa pikwa."
Share:

LEMA AMPELEKA MWIGULU KWA RAIS


Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amemuomba Rais John Magufuli kutafakari upya kama Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, bado anafaa kuongoza Wizara hiyo, kufuatia wimbi la matukio yanayoashiria ukosefu wa usalama nchini.

Lema, ambaye ni waziri kivuli wa wizara hiyo, alisema hayo jana, wakati akizungumzia kauli za Mwigulu aliyoitoa juzi kuhusu kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) na matukio mengine, yakiwamo ya kupotea kwa aliyekuwa msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Ben Saanane.

“Jana (juzi) nilifikiria Mwigulu angeachana na ngonjera zake akaongelea habari angalau ya maslahi ya askari hawa, Mwigulu amenisikitisha sana, na sidhani kama anastahili kukaa kwenye ile ofisi hata kwa saa mbili.

“Yeye kama Waziri wa Mambo ya Ndani, tangu Lissu ameshambuliwa hajawahi kurusha hata mguu Nairobi, hata kwenda kuongea na Waziri wa Mambo ya Ndani Kenya, kuomba ulinzi kwa ajili ya mgonjwa.

“Wakati ni mbunge mwenzake, tena wa mkoa wake amepigwa risasi, ila hajishulishi, jana anaongea vitu vyepesi kuhusu maisha ya watu, kwa kauli zake kama

kuna mtu alimtazama wakati anaongea, utajua tukio la Lissu limefanywa na nani, na nani yuko nyuma ya tukio hili, vinginevyo angekuwa na ujasiri wa kuelekeza polisi kutafuta wahalifu kwa nguvu zote, angewaza pengeni anayefuata ni yeye,” aliongeza.

“Serikali ijue tu kama tukio hili la Lissu haliko connected na wao, waliofanya tukio hili wana nia mbaya,” alisema Lema.
Share:

Saturday, 30 September 2017

POLEPOLE AFUNGUKA SABABU ZA KUFUTA UCHAGUZI KASKAZINI

Dar es Salaam. Chama cha Mapinduzi (CCM), kimesema Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana hajahudhuria vikao vya kamati kuu na halmashauri kuu kwa kuwa aliomba udhuru wa kihali kwa kuwa anauguza ndugu yake wa karibu wa familia.
"Ndugu yetu Kinana anauguza ndugu yake wa karibu, tumwombee apone lakini Kinana alishiriki vyema kikao cha Sekretarieti. Kinana hajajiuzulu au kuandika barua ya kujiuzulu," amesema Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole.

Chama hicho pia kimetangaza kuwachukulia hatua kali makada wake watakaobainika kukiuka utaratibu wa uchaguzi wa ndani wa chama hicho.

Polepole amesema hayo leo Jumamosi alipozungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za chama hicho Lumumba jijini hapa akitoa taarifa ya vikao vya juu vilivyoanza juzi Ikulu ya Dar es Salaam. Amesema Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli amesema vikao hivyo vimepitisha majina ya wagombea wa uenyekiti ngazi ya wilaya.

Amesema kati ya wilaya 161 za kiserikali ambazo ni sawa na za kichama, kikao cha Kamati Kuu na Halmashauri Kuu iliyoketi leo Jumamosi  imezuia uchaguzi katika wilaya sita.

Amezitaja wilaya hizo kuwa Moshi Mjini, Siha, Hai na Makete kwa sababu waliojitokeza kugombea wameonekana kuwa watu hatarishi kwa chama hicho na uchaguzi utatangazwa baadaye.

Wilaya za Musoma Mjini na Musoma Vijijini zitarudia baada ya kutenganishwa kutoka wilaya moja na kuwa mbili.

"Chama hakitasita kuwachukulia hatua kali ikiwemo kufuta uchaguzi au kuwafukuza uanachama wale wote watakaobainika kutozingatia maadili na kanuni za chama chetu," amesema Polepole.

Amesema Halmashauri Kuu imetoa onyo kali kwa wanachama wa Zanzibar walioanza kampeni za uchaguzi mkuu ikisema muda bado na wakiendelea watachukuliwa hatua.

Mwananchi:
Share:

Friday, 29 September 2017

HIKI NDICHO KIMEFANYA GAZETI LA RAIA MWEMA LIFUNGIWE


LEO serikali imelifungia gazeti la Raia Mwema kwa kile kilichodaiwa kuwa limeandika taarifa zisizo za kweli kumuhusu Rais John Magufuli.
 

Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbas, ilidai kuwa gazeti hilo la kila wiki lilishindwa kupeleka uthibitisho wa taarifa hiyo.
 
 
Share:

MBOWE KUPOKONYWA GARI BUNGE LASEMA HIVI

OFISI ya Bunge imesema Kiongozi wa Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe hajanyang’anywa gari.
Taarifa iliyotolewa na Bunge leo Alhamisi imesema kilichotokea ni kwamba, gari hilo limerudishwa nchini ili dereva afuate utaratibu wa kupata kibali cha kusafiri nje ya nchi.
Mbowe yuko Nairobi nchini Kenya ambako Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anaendelea na matibabu baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Septemba 7 akiwa nyumbani kwake Area D mjini Dodoma.
Bunge limesema ni kweli gari lenye namba ya usajili STL 4587 aina ya Toyota Prado limetengwa maalumu kwa ajili ya kumuhudumia Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika kutekeleza majukumu yake ya kikazi na binafsi nchini.
“Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni aliomba gari ikamhudumie mjini Nairobi nchini Kenya na Ofisi ya Bunge iliridhia ombi hilo na kuomba taratibu zizingatiwe. Hata hivyo, ofisi iligundua kwamba gari ilikwenda Nairobi na dereva hakupata kibali cha kusafiri nje ya nchi ambacho kila mtumishi wa umma anayesafiri nje ya nchi lazima apate kibali hicho kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi,” imesema taarifa ya Bunge.
Bunge katika taarifa hiyo limesema kwa kuwa utaratibu haukukamilika, dereva aliambiwa alirejeshe gari hilo nchini na kuliegesha katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha hadi utaratibu mwingine utakapokamilika.
“Dereva yupo Dodoma anakamilisha taratibu ili ofisi iweze kumuombea kibali Ikulu ndipo anaweza kurejea nchini Kenya kwa ajili ya kuendelea kumhudumia Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,” imesema taarifa.
Ofisi ya Bunge imesema inasikitishwa kutokana na utaratibu unaotumiwa na Ofisi ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wa kuzungumzia masuala yanayohusu ofisi hiyo kupitia kwa msemaji wa chama kama inavyoonekana kwenye mitandao ya kijamii akitoa malalamiko kwa niaba ya ofisi hiyo.
“Ni vyema ikaeleweka kwamba Ofisi ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ni kama ofisi nyingine zinazohudumiwa na Sekretarieti ya Bunge ambayo inapaswa kufuata kanuni na taratibu za uendeshaji wa Ofisi na ni kosa kwa mtumishi kwenda kinyume na masharti ya Utumishi wa Umma,” taarifa hiyo imesema.
Imeelezwa katika taarifa kuwa ni dhamira ya Ofisi ya Bunge kuendelea kumhudumia Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa kufuata misingi na kanuni za utumishi wa umma na zile za Bunge bila kuchanganya na siasa.
“Ofisi ya Bunge inauhakikishia umma kuwa taratibu zikishakamilika Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ataendelea kuhudumiwa popote atakapokuwa,” imesema taarifa hiyo.
Share:

MBUNGE LIJUALIKALI YAMKUTA

Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali na viongozi watatu wa Chadema wilayani Malinyi wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kufanya kusanyiko lisilo halali.
Mbunge huyo amekamatwa leo Alhamisi saa 12:40 jioni akitoka kwenye kikao cha ndani cha chama hicho kilichofanyika katika Kijiji cha Makerere wilayani Malinyi.
Akizungumzia kukamatwa kwa viongozi hao, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati, Alfonce Mbassa amesema baada ya kumaliza kikao, mbunge huyo na viongozi wengine walipanda kwenye magari ili  kuondoka lakini ghafla lilitokea gari la polisi na askari walimuamuru Lijualikali ashuke.
“Tulishuka wote kujua tatizo ni nini lakini askari walimhoji Lijualikali kwa nini amekwenda kufanya siasa Malinyi wakati yeye ni mbunge wa Kilombero,” amesema Mbassa.
Amesema walijaribu kuwaelewesha polisi kwamba kilikuwa ni kikao cha ndani lakini askari walisisitiza kuwa lilikuwa kusanyiko lisilo halali.
Amewataja waliokamatwa pamoja na mbunge huyo kuwa ni Mwenyekiti wa Chadema Malinyi, Emmanuel Lukindo; Katibu wake, Sadi Lyampawe na Katibu wa Uenezi wa wilaya, Lucas Lyambalimu.
“Lakini tulivyowabana polisi wametuambia wameelekezwa na Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Majura Kasika kuwakamata,” amesema Mbassa.
Alipotakiwa kuzungumzia tuhuma hizo, mkuu wa wilaya Kasika amesema ni kweli ameagiza polisi kumkamata mbunge huyo kwa kuwa anafanya siasa nje ya jimbo lake.
“Ndiyo, nimetoa maelekezo akamatwe maana hakuna mbunge anayeruhusiwa kufanya siasa nje ya jimbo lake na tunaendelea kumshikilia kwa mahojiano,” amesema Kasika.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leons Rwegasira amesema hajapata taarifa za kukamatwa kwa mbunge huyo.
“Nipe muda nifuatilie nitakujulisha maana bado sijapata taarifa za kukamatwa kwa mbunge huyo,” amesema Rwegasira.
Share:

Thursday, 28 September 2017

KUHUSU GARI LILILOKUWA LIKIMFUATILIA LISSU MWIGULU ASEMA HAYA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu amesema leo kuwa baada ya polisi kufuatilia gari hiyo wamegundua iliyokuwa inamfuatilia Lissu ilikuwa na namba batili huku gari halisi yenye namba hizo za usajili ikiwa Arusha.
“Utoaji wa taarifa na wenyewe haukuwa rasmi kwa mfano Lissu aliposema kuna gari inamfuatilia nilielekeza polisi wakaifuatilia ikakutwa Arusha kuna gari ndogo ya namba hizo kwa hiyo kuna moja iliweka namba batili.
“Ile gari ilikutwa kule kule na haikuwa na ruti ya huku (Dar es Salaam) huwa iko kule kule, kwa hiyo kwenye mambo haya ndiyo maana tunahitaji sana ushirikiano.
“Natamani watu hawa tungewatia nguvuni pale pale ningepewa ‘tip’ mapema tungefuatilia hili na kitendawili cha watu wasiojulikana tungekitegua mara moja,” amesema Mwigulu akihojiwa na Kituo cha Televisheni cha Clouds, leo.
Pamoja na mambo mengine amesema Lissu mwenyewe anaweza kusaidia uchunguzi katika tukio hilo ambapo pia ameonya watu watu wanaotengeneza matukio ya aina hiyo kufikiria madhara yanayoweza kutokea baada ya tukio.
Share:

Sunday, 24 September 2017

MKE WA LISSU ASEMA HAYA

Nairobi. Kwa mara ya kwanza, Alicia Magabe ambaye ni mke wa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amezungumzia tukio la mumewe kushambuliwa kwa risasi na kudokeza kwamba haliwezi kuwa limetokana na sababu nyingine isipokuwa kazi ambazo amekuwa akizifanya.
Pia amezungumzia kuhusu afya yake na kueleza kuwa bado siyo nzuri na kuwaomba Watanzania waendelee kumuombea.

Mbali ya Alicia ambaye pia ni mwanasheria, dereva wa Lissu naye amezungumza akisema ameathiriwa kwa kiasi kikubwa na tukio hilo huku akiahidi kuripoti polisi mara baada ya kurejea nchini.

Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), amelazwa katika Hospitali ya Nairobi tangu alipopelekwa huko baada ya kupigwa risasi akiwa ndani ya gari nje ya nyumba yake mjini Dodoma mchana wa Septemba 7 akitokea bungeni.

“Watanzania wote wanajua Lissu maisha yake yote amekuwa ni mtetezi wa wanyonge na tukio hili amelipata kutokana na kazi zake hizo hivyo nawaomba tumuombee tu,” alisema.

“Ninachoweza kusema hali ya mheshimiwa Lissu sio nzuri ingawa ni tofauti na tulivyomleta hapa, hivyo naomba Watanzania kuendelea kumuombea.”

Aliwashukuru Watanzania kwa michango, na maombi yao kwa Lissu akisema hiyo inaonyesha ni jinsi gani wanathamini mchango wake kwa jamii.

Alipoulizwa kuhusu kauli ya Serikali kwamba ipo tayari kugharimia matibabu ya Lissu popote ikiwa itaombwa na familia hiyo, Alicia ambaye pia ni wakili alisema kwa sasa hana maoni.

“Katika hili no comment (sina maoni) ndio tumesikia jana amezungumza na kwa kuwa jambo hili siyo la uamuzi wa mtu mmoja, mimi sina cha kusema,” alisema.

Hata hivyo, alisema anashukuru kazi kubwa ambayo inafanywa na madaktari wa Hospitali ya Nairobi na kusema wanaridhishwa na matibabu ambayo anapatiwa kwa sasa.

Dereva wa Lissu azungumza

Mbali ya Alicia, dereva wa Lissu ambaye ndiye mtu pekee waliyekuwa wote si ya tukio hilo, Simon Bakari naye alizungumza kwa mara ya kwanza kuhusu tukio hilo na kudokeza kwamba limevuruga na hana kumbukumbu sahihi.

Dereva huyo ambaye naye anaendelea kupatiwa matibabu ya kisaikolojia katika hospitali hiyo ya Nairobi alisisitiza, “Kwa sasa siwezi kuzungumza vizuri tukio hili kwani nadhani sina kumbukumbu vizuri.”

Alipoulizwa kuhusu wito wa polisi wa kwenda kutoa maelezo, alisema atafanya hivyo pindi atakaporejea nchini baada ya matibabu.

“Nilisikia polisi wamenitaka nikatoe maelezo lakini sijisikii vizuri na bado napata matibabu. Nitakwenda,” alisema.

Mwananchi:
Share:

MSIGWA AUKWAA UGOMVI WA MSUKUMA NA RPC

Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA Peter Msigwa amezidi kushikilia suala la Mbuge wa Geita Mjini na RPC wa Geita na kusema kuna jambo kati yao lakini anashindwa kuelewa inakuaje mbaka sasa TAKUKURU inashindwa kuwahoji wote wawili.
Msigwa amesema hayo kupitia mtandao wake wa Twitter zikiwa zimepita siku kadhaa toka Mbunge na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita, Joseph Msukuma kudai kuwa ana siri nyingi za Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo na kudai atazitoa siri hizo ikiwa Kamanda wa Polisi huyo hatamuomba msamaha kwa kitendo alichomfanyia ikiwa pamoja na kumkamata na kumlaza rumande.

"Msukuma amesema anajua siri za RPC wa Geita , TAKUKURU kwa nini hamjiongezi kuwahoji wote wawili, kuna kitu hakipo sawa kinaendelea hapa" aliandika Mchungaji Msigwa
Mbunge wa Geita alikamatwa na jeshi la polisi na kulazwa rumande kwa masaa 24 kufuatia vurugu zilizofanywa katika mgodi wa Geita Gold Mine (GGM) lakini alipotoka Mbunge huyo alianza kumshtumu RPC wa Geita na kusema anafahamu mambo yake mengi, akahitaji kuombwa msamaha ndani ya siku tatu na RPC huyo huku akiahidi kutoa siri zake kama hatafanya hivyo.
Share:

Friday, 22 September 2017

NDUGAI AMJIBU MBOWE HAYA KUHUSU SH.43M ZA WABUNGE KUMTIBU LISSU

Spika Job Ndugai na Freeman Mbowe (Picha na maktaba).
OFISI ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeijibu kauli ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye mapema leo akizungumza na wanahabari alisema Spika Job Ndugai amezuia Sh. Milioni 43 zilizochangwa na wabunge kusaidia matibabu na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anayetibiwa Nairobi Kenya baada ya kupigwa risasi.
Ofisi hiyo imeeleza katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa, michango ya wabunge kusaidia matibabu ya Tundu Lissu tayari zimeshatumwa Nairobi Hospital anakotibiwa mbunge huyo.
Taarifa ya ofisi ya Spika inasema kuwa fedha hizo zimetumwa siku ya tarehe 20 Septemba, 2017 kupitia benki ya Barclays Tawi la Huriringham akaunti namba 045 11553318.

Share:

Wednesday, 20 September 2017

HAYA NDIYO MAAMUZI YA MAHAKAMA JUU YA VIGOGO WA MRADI WA MABASI YA MWENDOKASI

MAHAKAMANI ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru vigogo watatu wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), akiwemo mtendaji mkuu wa mradi huo, Asteria Mlambo na mwenzao.
Akitoa hukumu hiyo leo Jumatano ni Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage amesema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi 10 wa upande wa mashtaka, vielelezo na ushahidi wa upande wa utetezi ameona upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakabili vigogo hao pasipo kuacha shaka.
Mbali na Mlambo wengine walioachiwa huru ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Evodius Katale, Mwanasheria Mkuu wa DART, Francis Kugesha na mkurugenzi wa kampuni ya Yukan, Yuda Mwakatobe.
Washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi kwa kula njama, kusababisha hasara ya Sh 83.5 milioni.
Katika kesi hiyo ilidaiwa kuwa Septemba Mosi na Oktoba Mosi, mwaka 2013 maeneo ya Kinondoni Dar es Salaam, Mlambo, Katale na Kugesha wakiwa wafanyakazi wa mradi huo, walishindwa kutekeleza majukumu yao vizuri na kuisababishia Serikali hasara ya Sh 83.5 milioni.
Share:

Tuesday, 19 September 2017

ZITTO ADAI ANAJIHISI KAMA MWENDAWAZIMU


Zitto Kabwe akikagua gofu la nyumba yake iliyoteketea kwa moto kigoma.
KIONGOZI wa ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma mjini, Mh. Zitto Kabwe amefunguka na kusema kwamba uchungu anaoupata baada ya nyumba yake ya kwanza kuungua moto umemfanya kuwafikiria wananchi wanaobomolewa nyumba zao bila fidia.
Zitto amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa Facebook baada ya kutazama nyumba yake ya kwanza iliyoteketea kwa ajali ya moto mwishoni mwa wiki iliyopita.
“Sikudhani kabisa kuwa naweza kuumizwa na kupata uchungu kwa tukio kama hili na ninajiuliza huu uchungu ni wa nini? Kumbe ni uchungu wa nyumba ya kwanza. Nawafikiria wananchi wenzangu wanaobomolewa nyumba zao bila fidia, na wengi ni nyumba zao za kwanza na pekee. Uchungu wao nausikia. Hasira zao nazihisi,”  Zitto ameandika.
Ameongeza kuwa “Nafikiria wanaobomolewa maeneo ambayo yamekuwa sehemu ya maisha yao na kuwapa kipato na familia zao. Nausikia uchungu wao. Sio uchungu wa nyumba ya kwanza. Uchungu wa kupoteza kabisa walichonacho na pengine kupoteza matumaini ya maisha.”
Pamoja na hayo Zitto amesema kuwa ameridhika kwamba kilichotokea kwenye nyumba yake kuungua moto ni ajali ya kawaida na wala watu wasichukulie kwa muktadha wa matukio yanayoendelea nchini kwetu hivi sasa.
“Ni ajali na funzo ni kuchukua tahadhari zaidi. Hasara ni kubwa sana lakini muhimu ni kuwa maisha yanaendelea na Mungu ataleta uwezo wa kuendeleza mengine. Nilipata salaam kutoka kwa watu wengi na napenda kuthibitisha kuwa ni ajali tu,” Zitto.
Mbali na hayo Mh. Zitto Kabwe amesema kuwa nyumba yake imeungua siku moja baada ya yeye kuondoka Kigoma na akiwa njiani kuelekea nchini Kenya ndipo alipatiwa taarifa kuhusu ajali hiyo. 
“Ajali imetokea siku moja tu baada ya mimi kutoka Kigoma, Septemba 15 ,  2017. Hata hivyo muda wote wa siku 2 nikiwa nje ya Kigoma, sikupata hisia kabisa. Labda ni kwa sababu ya safari yangu ya Kenya ambayo nayo haikuwa ni kwa jambo la kawaida” Zitto.
Aidha Mh Zitto ameongeza “Leo asubuhi nimeamka na kurudi kutazama nyumba hii. Imekwisha yote nimezunguka zaidi ya mara 3 kutazama gofu lile lile nililotazama jana baada ya kufika. Nimechungulia chumba nilichokuwa nalala zaidi ya mara moja. Nipo kama mwendawazimu,” alisisitiza Zitto Kabwe.
Nyumba ya Zitto Kabwe iliyoungua huko Mwandiga mkoani Kigoma inadaiwa ndiyo nyumba yake ya kwanza baada ya kupata  ridhaa ya kuwa mbunge

Share:

Sunday, 17 September 2017

ACACIA WAHITIMISHA KWA SHEREHE

Wafanyakazi wakiendelea kufanya maandalizi kwa ajili ya kuwaaga wafanyakazi wenzao jana.
Muonekano wa viti watakavyokaa wafanyakazi wa Acasia.
Magari yakiwa yamepaki jana.
Acacia yakamilisha usitishaji wa uchimbaji mgodi wa Bulyanhulu. Mgodi huo umepunguza wafanyakazi 1,200, wakandarasi 800, sasa wamebaki wafanyakazi 200.
Ilielezwa kuwa sababu ya kuwapunguza wafanyakazi hao ni kutokana na mwenendo wa soko la madini kutikisika.
Share:

Saturday, 16 September 2017

BALOZI KUMPELEKA JPM MAREKANI

Kaimu balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt Inmi Patterson amesema kuwa angependa kumpeleka rais John Pombe Magufuli nchini Marekani kwa ziara ya wiki tano.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, alitoa matamshi hayo mjini Dar es Salaam hivi majuzi wakati wa sherehe fupi ya kumkaribisha afisa wa maswala ya umma katika ubalozi huo Bi Bribille Ellis.
''Mwalimu Nyerere alitembelea Marekani miaka 1960 kwa ziara ya wiki tano.
Wiki tano ni wakati mrefu na aliweza kutembelea miji kadhaa...Ningependa kumpeleka rais Magufuli kwa ziara ya wiki tano nchini Marekani'', alisema na kuvutia kicheko kutoka kwa umma uliokuwepo.
Gazeti hilo lilimnukuu bi Patterson akisema kuwa katika uzoefu wa uongozi na programu za kubadilishana kama zile zilizotekelezwa na Mwalimu Nyerere 1960 zimefuatiliwa kwa sababu zilikuwa muhimu katika kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na Tanzania.
Akimnukuu mtangazaji maarufu wa redio nchini Marekani, Edward Murrow, Bi Patterson alisema kuwa kwa uhusiano wa taasisi na mataifa kuimarika , lazima uanze katika kiwango cha kibinafsi.
Rais Magufuli hajawahi kutembelea taifa lolote nje ya Afrika tangu alipochaguliwa kuwa rais mnamo mwezi Oktoba 25.
Amekuwa akisisitiza kwamba ana kazi nyingi za kufanya nchini na kwamba kile ambacho kinaweza kufanywa kimataifa kinaweza kufanywa na mabalozi wa Tanzania waliopo mataifa hayo.
Share:

MBUNGE WA CCM ASEMA HAYA BAADA YA KUMTEMBELEA LISSU

Tundu Lissu.
MBUNGE wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu (CCM) amemtembelea Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu aliylazwa katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya akitibiwa majeraha baada ya kushambuliwa kwa risasi wiki iliyopita nyumbani kwake, Area D, Dodoma.
Nyalandu ameandika;
“Nimefika Hospitali ya Nairobi mapema leo kumjulia hali Mh. Tundu Lissu. MADAKTARI wanaendelea kumfanyia matibabu, na bado hatujaruhusiwa kumuona.
“Kwa niaba ya Wana-Singida, na Watanzania wote, nimetoa salaam za pole kwa mke wake, na bado nasubiri uwezekano wa kuweza kuonana naye usiku wa leo endapo MADAKTARI wataruhusu.
“Cha muhimu zaidi, SOTE tuendelee KUMWOMBEA. MUNGU amtendee wema, na kumponya katika majira haya ya kujaribiwa kwake. Katika yote ndani ya yote, IKAWE HERI KWAKE. (Pichani na mdogowangu Peter Nyalandu, The Nairobi Hospital, Kenya).”
Nyalandu ameungana na Wabunge wa CHADEMA wakiwemo Freeman Mbowe, Godbless Lema, Joshua Nassary, Peter Msigwa na mbunge wa zamani Ezekiel Wenje, ambao nao wapo Nairobi kuangalia hali ya mgonjwa huyo.

Share:

Friday, 15 September 2017

WAZEE WA KIGOMA WAMTOLEA UVIVU JOB NDUGAI


Wazee wa Kigoma wakiwakilishwa na Mwenyekiti wa Ngome ya Wazee ya Chama cha ACT Wazalendo, Alhaj Jaffar Kasisiko wamesikitishwa na kauli aliyotoa Spika Ndugai kuwa anaweza kumzuia Zitto Kabwe asiongee chochote mpaka ubunge wake utakapokwisha.

Wazee hao wanasema kitendo cha Spika kumzuia Zitto Kabwe kuongea bungeni ni sawa na kuwazuia wao wasiongee na shida zao zisiweze kutatuliwa na kudai inaonekana hiyo kauli imeshafanyiwa kazi na kitendo cha kumwita Zitto kwenye Kamati ni sawa na kupoteza muda tu na kudai jambo hilo halimtendei haki kijana wao Zitto Kabwe na wao wenyewe.

Aidha wazee hao wamemtaka Spika Job Ndugai na viongozi wengine wasiwe na kibri na watazame mambo ambayo yanawaonganisha kwa pamoja.

Share:

Ads

Blog Archive