OFISI ya
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeijibu kauli ya Mwenyekiti wa
Chadema, Freeman Mbowe ambaye mapema leo akizungumza na wanahabari
alisema Spika Job Ndugai amezuia Sh. Milioni 43
zilizochangwa na wabunge kusaidia matibabu na Mbunge wa Singida
Mashariki, Tundu Lissu anayetibiwa Nairobi Kenya baada ya kupigwa
risasi.
Ofisi hiyo
imeeleza katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa, michango ya
wabunge kusaidia matibabu ya Tundu Lissu tayari zimeshatumwa Nairobi
Hospital anakotibiwa mbunge huyo.
Taarifa ya ofisi ya Spika inasema kuwa fedha hizo zimetumwa siku ya
tarehe 20 Septemba, 2017 kupitia benki ya Barclays Tawi la Huriringham
akaunti namba 045 11553318.
0 comments:
Post a Comment