Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limezikumbusha klabu zote ambazo
zinasimamiwa na shirikisho hilo kuhakikisha zinamaliza zoezi lake la
usajili mapema.
TFF imetoa tamko hilo kupitia kwa Ofisa Habari, Alfred Lucas kuwa
katika timu 16 za Ligi Kuu ya Tanzania Bara ni mbili pekee ndizo ambazo
zimewasilisha majina yao ya usajili kuelekea msimu ujao wa 2017/18.
Katika majina ya klabu hizo, Simba na Yanga siyo miongoni mwao, hiyo
inamaana kuwa kumbe hata wachezaji wao wapya waliosajiliwa hivi karibuni
bado hawatambuliki ndani ya mfumo wa usajili wa shirikisho hilo.
Baadhi ya wachezaji waliosajiliwa hivi karibuni ni Emmanuel Okwi kwa upande wa Simba na Ibrahim Ajibu upande wa Yanga.
Alfred amesema timu 24 za Ligi Daraja la Kwanza na 24 Ligi Daraja la
Pili zinatakiwa kukamilisha mfumo wa usajili kwa kuwa imesalia wiki moja
tu kabla ya mfumo kufungwa.
Dirisha la usajili lilifunguliwa Juni 15, mwaka huu na litarajia kufungwa Agosti 6, mwaka huu
0 comments:
Post a Comment