WAKATI waandishi wakijaa kwenye Uwanja wa ndege wa ere, kumsubiri
kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi, Katibu Mkuu wa timu hiyo, Charles Mkwasa, amesema mawasiliano na staa huyo yamepotea.
Awali ilitangazwa kuwa mchezaji huyo raia wa Congo DR angetua nchini
saa nane za mchana huu, lakini hadi sasa hajatua na katibu huyo amesema
mwanzo walikuwa na mawasiliano naye lakini ghafla yamepotea na hawajui
atatua saa ngapi.
“Sijui atatua saa ngapi, tumepoteza mawasiliano naye tukimtafuta
hatumpati, hivyo kama atakuja baadaye basi tutawataarifu,” alisema
Mkwasa.
0 comments:
Post a Comment