Aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuph Manji, akiongozana na polisi
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam leo limemkabidhi
mfanyabiashara, Yusuf Manji na wenzake kwa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu baada ya kumaliza upelelezi wao wa kumhoji katika kesi ya uhujumu
uchumi inayomkabili yeye na wenzake.
Akizungumza wakati wa kesi hiyo, Wakili wa Serikali, Mutalemwa
Kishenyi, amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, kuwa washtakiwa
hao wamerudishwa tena Mahakamani ilivyokuwa imeamuru warudishwe baada ya
Polisi kumaliza mahojiano yao.
Naye, Hakimu Shaidi alisema kesi hiyo itaendelea na utaratibu kama
ilivyokuwa mwanzo na hivyo ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 8, mwaka
huu.
Jana Mahakama hiyo iliruhusu Yusuf Manji na wenzake watatu kwenda
kuhojiwa na Polisi kwa lengo la kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo.
0 comments:
Post a Comment