ALIYEKUWA mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Hashim
Rungwe Spunda anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa siku nne sasa.
Rungwe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Umma (Chaumma) anashikiliwa
katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam
akituhumiwa kughushi nyaraka.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa
amesema leo Septemba 5 kuwa, Rungwe anashikiliwa kituoni hapo kwa siku
nne.
Hata hivyo, Kamanda Mambosasa hakutaka kuingia kwa undani kuhusu suala hilo akisema hana taarifa za kutosha.
0 comments:
Post a Comment