KIUNGO wa Simba, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, amesema kuwa, endapo muunganiko wa Donald Ngoma, Obrey Chirwa, Papy Tshishimbi na Thabani Kamusoko utatimia, basi kuna uwezekano mkubwa wa kuipa ubingwa timu yao ya Yanga.
Niyonzima ambaye Jumamosi iliyopita
aliichezea Simba mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara tangu ajiunge
nayo akitokea Yanga, amesema pamoja na timu yake hiyo kupata ushindi wa
mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting, wanaweza kukutana na
kikwazo cha kuwa mabingwa kutoka kwa Yanga kwa kuwa wanaonekana wapo
vizuri sana tofauti na watu wanavyodhani.
Akizungumza na Championi Jumatano, Niyonzima
amesema kuwa watu wengi wameanza kuonyesha wazi kuibeza Yanga kutokana
na sare iliyoipata Jumapili dhidi ya Lipuli ya Iringa, jambo ambalo
kwake haoni ni sawa kwani anaamini Yanga bado ina kikosi kizuri.
“Mbali na hao, pia watu wanatakiwa
kukubaliana na mimi kuwa Ngoma ni mchezaji mzuri na msumbufu sana
uwanjani, hivyo atakapopona Chirwa na Tambwe, hakika watatusumbua sana
tofauti na wengi wanavyodhani kwamba kutoka sare kwa Yanga kutaifanya
ishindwe kutetea taji lake.
“Kikubwa mimi ninachoweza kukisema hapa
klabu yangu ya Simba inatakiwa tulitambue hili na tuendelee kukaza kila
mchezo wetu ili tuweze kuibuka na pointi tatu muhimu kwani njia pekee
ya kufikia mafanikio tuliyojipangia ni kuendeleza kuvuna ushindi katika
kila mechi iliyo mbele yetu na tuachane na kuwabeza Yanga ambao mimi
nafahamu uzuri wao ulipo.
“Kwa sasa utaona Yanga inateseka kupata
mabao kutokana na nafasi ambayo Ngoma amekuwa akichezeshwa pamoja na
Raphael Daudi, ila atakapokuja kuanza Chirwa ambaye ni msumbufu kama
yeye hakika timu yao itabadilika,” alisema nahodha huyo wa Rwanda.
0 comments:
Post a Comment