Pamoja
timu za Simba na Yanga ziko sawa kipointi, lakini kiungo wa Simba,
Haruna Niyonzima ameibuka na kusema kuwa hawatakiwi kulinganishwa na
Yanga kwa sasa badala yake mashabiki wanatakiwa kuwapima uwezo wao baada
ya kupita michezo mitano ijayo ya ligi kuu.
Niyonzima,
raia wa Rwanda, amesema hayo wakati kikosi chao kikilingana pointi na
Yanga, wote wakiwa na pointi nne baada ya michezo miwili ya ligi lakini
wao wapo juu kutokana na idadi kubwa ya mabao waliyonayo.
Niyonzima
keshokutwa Jumapili atakuwa sehemu ya wachezaji wa Simba ambao
watashuka dimbani kucheza mchezo wa tatu wa ligi wa timu hiyo dhidi ya
Mwadui FC ya Shinyanga, mechi ambayo inatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja
wa Uhuru, Dar.
Mnyarwanda
huyo amesema kuwa ni mapema mno kuanza kuwajaji juu ya uwezo wao mbele
ya mahasimu zao hao lakini ukweli wa kila kitu utajulikana baada ya
kupita kwa mechi hizo tano zijazo za ligi kuu.
“Yanga
ni timu nzuri na kila mmoja analijua hilo kwani wamesajili wachezaji
ambao wamewaongezea kitu ndani yao na nilishasema tangu zamani kuwa ni
timu nzuri na bora, lakini suala la kuanza kutulinganisha nao nadhani
hilo kwa sasa mashabiki wanatakiwa waliweke pembeni.
“Nadhani
itakuwa vizuri kama tutaanza kulinganishwa na timu zote za ligi kuu
baada ya michezo mitano ijayo, ambapo michezo hiyo ndiyo itaamua ni nani
yuko vizuri kuliko mwenzake na hapo ndipo itakuwa kipimo bora zaidi
kwetu na kwao kuliko ilivyo hivi sasa,” alisema Niyonzima.
SOURCE: CHAMPIONI
0 comments:
Post a Comment