Thursday, 14 September 2017

YANGA WAFUNIKA TEN ASEMA HAYA

 
Mashabiki wa Yanga kutoka Njombe, Makambako na mikoa mingine ya jirani wamejikusanya na kuipa timu hiyo fedha ya maana.
Mashabiki hao wameitana kwenye kikao cha pamoja mkoani Njombe na kuchanga fedha ambazo huenda zikatosha kugharamia kambi ya Yanga Njombe.
Mbali na mashabiki hao, wikiendi iliyopita wanachama wa Ubungo Terminal walitoa pia kiasi cha Sh500,000 kama posho kwa timu nzima baada ya ushindi dhidi ya Njombe.
Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amekiri klabu yao kupokea fedha hizo na kuwasifu mashabiki kwa moyo huo wa uzalendo.
"Tunashukuru ni kitu kizuri kwa klabu. Tunafurahi kuona wanatujali na kutupa michango," alisema Ten.
"Tunawapongeza na kuwapa wengine hamasa ya kuendelea kuisapoti timu," aliongeza ofisa huyo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive