Sunday, 10 September 2017

UJUMBE WA MANARA YANGA

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amewapa vijembe watani wao Yanga baada ya kusema klabu hiyo isiwe na visingizio kwenda kucheza katika uwanja wa Chamazi.
“Sisi tumecheza hapa na hakuna tatizo lolote ambalo limetokea, mpira ulikuwa vizuri kwahiyo na hao wenzetu waje wasije wakaanza visingizio waje tu,” Manara.

Manara pia alilipongeza jeshi la Polisi kwa ulinzi jambo ambalo lilifanya mechi hiyo kumalizika bila kuwa na tatizo lolote.

“Ulinzi ulikuwa ni mzuri hakukuwa na tatizo lolote, kikubwa pongezi ziwaendee jeshi la polisi kwasababu wamejitahidi kufanya ulinzi.”

Azam na Yanga zitacheza katika uwanja wa Chamazi, Disemba 29 mwaka huu.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive