Sunday, 10 September 2017

ZITTO ABANWA KUHUSU BEN SAANANE


Mtumiaji mmoja wa Twitter anajiita @moringesokoine1 alimuuliza hivi "@zittokabwe Unakumbuka Tarehe 27/03/2013 Ulidai Mjumbe Wa Bavicha Ben Saanane Alitumwa Kukuwekea Sumu Kwenye Kinywaji Lunch Time Hotel?"

Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa twitter ameweka wazi msimamo wake huo wa kutoyumbishwa na watu hao ambao wameanza kusambaza taarifa mbalimbali kuhusu Zitto Kabwe na kusema hizo ni ajenda wanazofanya kutaka kumtoa kwenye mstari wa sakata kuhusu wahusika halisi ambao wamefanya shambulio la risasi kwa mbunge Lissu

"Hizi ni propaganda za dola ili kuhamisha mjadala kuhusu wahusika halisi wa shambulio la risasi dhidi ya Mbunge Tundu Lissu. Sitawapa muda" alisisitiza Zitto Kabwe 

Mbunge Zitto Kabwe amekuwa mstari wa mbele kulaani vitendo vya kinyama na kikatili ambavyo vimeanza kutokea Tanzania, kuanzia kuuawa kwa baadhi ya viongozi mbalimbali na askari polisi Kibiti Pwani mpaka katika shambulio lililompata Mbunge Tundu Lissu siku ya Alhamisi Septemba 7, 2017 mjini Dodoma baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive