Wednesday, 30 August 2017

SIMBA KUMPELEKA BEKI WA YANGA MAHAKAMANI

BUSWITA
Uongozi wa Simba umetangaza kumpeleka mahakamani beki Pius Buswita ambaye sasa yuko na klabu ya Yanga.


Simba imefikia uamuzi huo ikiwa ni siku kadhaa baada ya kiungo huyo kupatikana na hatia ya kusaini mbili na rungu la kukaa nje mwaka mmoja kumuangukia.
Mkuu wa kitengo cha habari cha Simba, Haji Manara amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kuona mambo hayaendi kiungwana.
"Buswita mwenyewe amekiri, amesema shetani sijui alimpitia. Lakini kuna watu wanafanya propaganda kwa kusambaza maneno ambayo si sahihi hata kidogo.
"Wanataka kuitisha TFF, wanataka kuichafua Simba wakati wanajua hili ni kosa la huyu kijana.
"Sisi tungekuwa tayari kumuachia kama suala la uungwana lingekuchukua nafasi. Lakini sasa watu wanalazmisha tuonekane wabaya, tutakwenda mahakamani kudai fedha zetu na sheria zaidi ichukue mkondo wake."
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive