Inawezekana watu wengi wanajiuliza mbona Farid Musa anaecheza
Tenerife, Hispania na Simon Msuva wa Difaa El Jadid ya Morocco
hawaonekani kwenye mazoezi ya timu ya taifa ‘Taifa Stars’? Wakati tayari
wachezaji wengine wapo kambini wakiendelea na mazoezi kuelekea mchezo
wa kirafiki wa kalenda ya FIFA dhidi ya Botswana siku ya Jumamosi
September 2, 2017.
Kocha mkuu wa Stars Salum Mayanga amefaganua ni kwa nini hadi sasa
Msuva na Farid bado hawajaonekana kwenye mazoezi ya timu ya taifa licha
ya kuwaita kwenye kikosi chake.
“Mpaka wakati huu tumebakiza wachezaji wawili ambao bado hawajafika
lakini Simon tunakamilisha ujio wake kwa sababu alipata tatizo kwenye
visa yake ambayo ilikwisha kule kwa hiyo leo tulikuwa tulibadilisha
tiketi yake kwa mara ya tatu lakini mpaka saa 5 ahubuhi kulikuwa na
uhakika wa kuanza safari yake leo”-Mayanga.
“Simon alikuwa na matatizo ya visa iliharibika kwa hiyo tulikata
tiketi ya kwanza ikasumbua, tukakata ya pili, lakini leo mida ya saa 4
alishapata visa yake na tulituma tiketi ya kuanza safari mchana wa leo
kuja huku kwa hiyo tunategemea kesho atawasili wakati wowote.”
“Farid amefika jioni hii na tayari yupo kambini, lakini Moreal ndiyo
mtu pekee ambae tunadhani hato hudhuria kwenye mechi inayokuja lakini
kwa asilimia 90 wachezaji wote wapo na tunaendelea vizuri na mazoezi na
maandalizi yetu.”
“Ni matumaini yangu kesho mchana tutaendelea na mazoezi katika hali
nzuri na keshokutwa asubuhi tutamalizia ili kusubiri mechi yetu dhidi ya
Botswana.”
0 comments:
Post a Comment