BEKI wa
zamani wa Simba, Frank Kasanga 'Bwalya' ameshauri nyota wa kikosi hicho
kwamba wapo vizuri kiuwezo, ila wanatakiwa kuwa watulivu na kujiamini
kile wanachokifanya uwanjani kwa madai watafika mbali.
"Sina
wasiwasi na uwezo wao ila wanatakiwa kuwa watulivu, waepuke papara,
mipira ya shoo badala yake wafanye kazi yenye madhara ya kuifanya timu
iweze kuwa na taswira ya ubingwa," alisema.
Amewaambia
wachezaji wa timu hiyo,kwamba wakifanikiwa kutwaa ubingwa msimu huu,
watakuwa wamejiandakia rekodi ya kutopata taji hilo ndani ya miaka
minne.
"Mchezaji mwenye mtazamo wa kufika mbali ni yule
anayehitaji kuweka alama kwa kila timu atakayoitumikia lakini kwa wale
ili mladi liende hawaoni hasara juu ya hilo, watwae ubingwa sawa
wakikosa sawa," alisema.
Staa huyo anasema ni wakati wa
wachezaji kulipa fadhira na kuelewa kwamba wamesajiliwa kwa kazi
maalumu akisisitiza kuwa kamati ya usajili ilitumia gharama tofauti na
misimu iliyopita ili kifanyike kitu tofauti na ligi zilizopita.
"Vitu
vingine vya kujiongeza wenyewe kama ni gharama za usajili vyombo vya
habari vimeweka wazi, hilo tu wanapaswa kulielewa kwamba ubingwa
unahitajika na siyo wao wajae upepo kujiona wapo juu ya malengo ya
klabu," alisema.
0 comments:
Post a Comment