Thursday, 21 September 2017

BAADA YA KUIKAZIA SIMBA KOCHA WA MBAO ASEMA HAYA



Kocha wa Mbao FC, Etienne Ndayiragije amesema, kikosi chake kilistahili ushindi katika mechi ya leo dhidi ya Simba.

Mbao FC imeibana Simba na kupata sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Ndayiragije raia wa Burundi, amesema kama wangeongeza umakini kidogo walikuwa na nafasi ya kufunga mabao zaidi.

“Tuliwabana Simba, tulicheza kwa mipango zaidi na kulikuwa na nafasi ya kushinda mechi ya leo. Lakini haikuwa hivyo, nawapongeza wachezaji wangu wamejitahidi na sasa tunaanza maandalizi ya mechi ijayo,” alisema.



Mbao FC ilionyesha soka safi na la ushindani na kufanikiwa kuibana Simba iliyopoteza nafasi nyingi za kufunga mabao.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive