Kaimu balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt Inmi Patterson amesema kuwa
angependa kumpeleka rais John Pombe Magufuli nchini Marekani kwa ziara
ya wiki tano.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, alitoa matamshi
hayo mjini Dar es Salaam hivi majuzi wakati wa sherehe fupi ya
kumkaribisha afisa wa maswala ya umma katika ubalozi huo Bi Bribille
Ellis.
''Mwalimu Nyerere alitembelea Marekani miaka 1960 kwa ziara ya wiki tano.
Wiki
tano ni wakati mrefu na aliweza kutembelea miji kadhaa...Ningependa
kumpeleka rais Magufuli kwa ziara ya wiki tano nchini Marekani'',
alisema na kuvutia kicheko kutoka kwa umma uliokuwepo.
Gazeti hilo
lilimnukuu bi Patterson akisema kuwa katika uzoefu wa uongozi na
programu za kubadilishana kama zile zilizotekelezwa na Mwalimu Nyerere
1960 zimefuatiliwa kwa sababu zilikuwa muhimu katika kuimarisha uhusiano
kati ya Marekani na Tanzania.
Akimnukuu mtangazaji maarufu wa
redio nchini Marekani, Edward Murrow, Bi Patterson alisema kuwa kwa
uhusiano wa taasisi na mataifa kuimarika , lazima uanze katika kiwango
cha kibinafsi.
Rais Magufuli hajawahi kutembelea taifa lolote nje ya Afrika tangu alipochaguliwa kuwa rais mnamo mwezi Oktoba 25.
Amekuwa
akisisitiza kwamba ana kazi nyingi za kufanya nchini na kwamba kile
ambacho kinaweza kufanywa kimataifa kinaweza kufanywa na mabalozi wa
Tanzania waliopo mataifa hayo.
0 comments:
Post a Comment