MBUNGE wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu (CCM) amemtembelea Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu aliylazwa katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya akitibiwa majeraha baada ya kushambuliwa kwa risasi wiki iliyopita nyumbani kwake, Area D, Dodoma.
Nyalandu ameandika;
“Nimefika Hospitali ya Nairobi
mapema leo kumjulia hali Mh. Tundu Lissu. MADAKTARI wanaendelea
kumfanyia matibabu, na bado hatujaruhusiwa kumuona.
“Kwa niaba ya Wana-Singida,
na Watanzania wote, nimetoa salaam za pole kwa mke wake, na bado
nasubiri uwezekano wa kuweza kuonana naye usiku wa leo endapo MADAKTARI
wataruhusu.
“Cha
muhimu zaidi, SOTE tuendelee KUMWOMBEA. MUNGU amtendee wema, na
kumponya katika majira haya ya kujaribiwa kwake. Katika yote ndani ya
yote, IKAWE HERI KWAKE. (Pichani na mdogowangu Peter Nyalandu, The
Nairobi Hospital, Kenya).”
Nyalandu ameungana na Wabunge wa
CHADEMA wakiwemo Freeman Mbowe, Godbless Lema, Joshua Nassary, Peter
Msigwa na mbunge wa zamani Ezekiel Wenje, ambao nao wapo Nairobi
kuangalia hali ya mgonjwa huyo.
0 comments:
Post a Comment