Saturday, 16 September 2017

HIVI NDIVYO CHIRWA, TSHISHIMBI WALIVYOTIKISA SONGEA


WAKATI Yanga inawasili Songea juzi Alhamisi, jezi ya kiungo Papy Kabamba Tshishimbi ndiyo iliyokuwa ikiuzwa kwa wingi, lakini jana Ijumaa jezi ya straika Obrey Chirwa nayo iliuzwa kwa wingi.


Chirwa amekuwa nje ya uwanja kwa muda akiuguza majeraha ya mi­suli ya mguu wake, lakini sasa yupo vi­zuri na anaweza kucheza mechi ya leo dhidi ya Majimaji.
Yanga leo inacheza na Majimaji mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Majimaji ikiwa imetoka kuifun­ga Njombe Mji bao 1-0 wikiendi iliyopita.

Katika mitaa mbalimbali ya Son­gea, wafanyabiashara ndogondogo wa­naonekana wakiwa na jezi zinazotumiwa na Yanga zenye jina na namba ya Tshishimbi na zile za Chirwa na wachezaji wen­gine wakiziuza kwa mashabiki.

Jezi hizo zinazouzwa nje ya utaratibu wa klabu, huuzwa kwa kati ya Sh 7000 hadi Sh 25,000 na mashabiki wamekuwa wakiz­ichangamkia kuzi­nunua.
Juzi jezi ya Tshishim­bi ilikuwa ikinunuliwa kwa wingi lakini jana Ijumaa ile ya Chirwa raia wa Zambia nayo ilinunuliwa kwa wingi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive