KUREJEA kwa mshambuliaji mwenye nguvu na kasi Mzambia, Obrey Chirwa
kumempa jeuri ya kufanya vizuri beki wa kati wa timu hiyo, Kelvin
Yondani katika mechi zao za Ligi Kuu Bara.
Mzambia huyo, alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu huku akikosa
michezo miwili ya ligi kuu kabla ya mchezo wa Njombe Mji kutokea benchi
dakika za mwishoni akichukua nafasi ya Donald Ngoma.
Chirwa alikuwa nje ya uwanja akiwa anasumbuliwa na maumivu ya nyama
za paja, aliukosa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba uliomalizika
kwa Yanga kufungwa kwa penalti.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Yondani alisema Chirwa ni kati ya
washambuliaji anaowakubali kutokana na aina yake ya uchezaji mbele ya
wapinzani wao. Yondani alisema
Chirwa si mwoga mbele ya mabeki wakorofi na wakati wote anajiamini,
hivyo anaamini kurejea kwake kutaimarisha safu yao ya ushambuliaji
inayoongozwa na Ngoma na Ibrahim Ajibu.
“Binafsi namkubali sana Chirwa na siku zote akiwepo yeye uwanjani basi ninakuwa na matumaini makubwa ya ushindi.
“Chirwa ni mchezaji anayejiamini na siyo mwoga kwa mabeki akiamua
jambo lake, huyu ni aina ya washambuliaji ninaowakubali kiukweli.
“Angekuwepo katika mechi ya Ngao ya Jamii (dhidi ya Simba) naamini
tungefanya vizuri,” alisema Yondani. Katika mechi hiyo ya Ngao ya Jamii,
Yanga ilifungwa kwa penalti 5-4 baada ya kutoka suluhu.
Stori: Wilbert Molandi
0 comments:
Post a Comment