Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe ameilalamikia benki kuu ya Tanzania
kwa hatua yake ya kutokutoa taarifa za hali ya uchumi za kila mwezi
(Monthly Economic Review) kama inavyoelekezwa na sheria ya benki kuu ya
mwaka 2006, Kupitia ukurasa wa Facebook wa Mbunge ameandika ujumbe
huu...
"Miezi 4 Benki Kuu ( BoT ) imekalia Taarifa nyeti za Uchumi ( MER ). Kinafichwa nini?
Benki Kuu ya Tanzania inapaswa, Kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya
mwaka 2006 ikisomwa pamoja na kanuni zake, kutoa Taarifa ya kila Mwezi
ya Mapitio ya Uchumi ( Monthly Economic Review).
Tangu nianze kusoma Taarifa hizi nikiwa Chuo Kikuu hii ni Mara ya
kwanza imepita miezi 4 MER haijachapishwa kwenye tovuti ya Benki Kuu ya
Tanzania. Mara ya mwisho imewekwa Taarifa ya Mwezi June inayoeleza
mapitio ya mwezi Mei 2017. Taarifa hiyo ya mwisho ilionyesha kuwa mauzo
yetu nje Kwa bidhaa za viwanda yameporomoka Kwa zaidi ya USD 700 milioni
sawa na Bombadier mpya 21 Hivi.
Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano ambayo imejiondoa kwenye Mpango wa
kuendesha Serikali Kwa Uwazi ( OGP ) na kujipa Sifa ya kufungia magazeti
kuliko Awamu yeyote tangu tupate Uhuru Sasa imeamua kutunyima na
Taarifa za kisheria kabisa kuhusu Uchumi.
Kwa kuchelewa huku, Taarifa itakayotoka lazima itakuwa ya kupikwa pikwa."
0 comments:
Post a Comment