Mwenyekiti
wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Kheri James amesema
kuwa CCM haina sababu ya kufanya kampeni katika uchaguzi Mkuu wa mwaka
2020 badala yake kuna kila sababu ya kupita bila kupingwa kutokana na
uimara wa CCM na serikali yake.
Kheri ameyasema hayo wakati
akizungumza na timu mbalimbali za kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani
wa Kata ya Kimandolu mkoani Arusha kutoka jumuiya za CCM.
Kheri amesema serikali ya awamu ya
Tano inayoongozwa na President Dr. John Pombe Magufuli imedhamiria
kutatua kero zote zisizo rafiki kwa wananchi kwa utekelezaji wa mkataba
wa wananchi na CCM kupitia ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020.
Amewafikishia wakazi wa Arusha salamu
za JPM kuwa anahitaji ushindi wa kishindo wa zaidi ya kura 12,000 na
hiyo itakuwa zawadi pekee kwake.
“Ndugu
zangu sisi wana CCM tunaweza kujadiliana harusi itafungwa vipi na wapi,
tunaweza tukajadiliana aina ya magari ya kununua lakini hatuwezi kuwa
na mjadala wa namna yoyote ile kwenye utafutaji wa dola ni lazima CCM
ishinde” -Kheri James
0 comments:
Post a Comment