Mbunge wa Muleba Kusini Profesa Anna
Tibaijuka amebainisha namna wanavyokabiliwa na changamoto katika
uendeshaji wa Shule ya Wasichana ya Kajumulo Alexander iliyopo Bukoba
baada ya mmoja wa wafadhili wa shule hiyo James Rugemalira kuwa
matatizoni.
Prof. Tibaijuka amesema hakuanzisha shule kibiashara badala yake
alijitoa kwa ajili ya kuwasaidia wasichana na kuwainua kielimu ndio
maana anajitoa kwa kile alichonacho kuwasaidia watoto hao kwa
kushirikiana na wafadhili wake huku akisema kuwa kwa sasa amebaki
mwenyewe katika kuchangia baada ya mfadhili wake mkubwa James Rugemalira
kushikiliwa na Polisi.
0 comments:
Post a Comment