Kama kuna mwanadamu mwenye bahati wiki hii baasi atakuwa ni Roberto
Lewandoski, mshambuliaji huyo wa Poland mambo yake yanaonekana
kumnyookea sana kuanzia ndani hadi nje ya uwanja.
Wakati Poland wakikipiga na Montenegro katikati ya wiki hi Lewandoski alifikisha idadi ya mabao 16 katika mechi za kufuzu kombe la dunia, idadi hiyo haijawahi kufikiwa na mchezaji yoyote katika mechi hizo.
Pia hattrick dhidi ya Almernia ilimfanya kufikisha mabao 50 katika timu yake ya taifa katika michezo 90, idadi hii ya mabao imevunja rekodi ya ufungaji Poland iliyokuwa ikishikiliwa na Wlodek Lubanski amabaye alifunga mabao 48 katika michezo 75.
Kama hiyo haitoshi lakini idadi hiyo ya mabao iliwafanya Poland kufudhu kwa ajili ya kombe la dunia litakalopigwa mwakani, safari ya Poland kwenda Urusi inakuja ikiwa ni baada ya kuikosa michuano hiyo mwaka 2010 na 2014.
Lakini jana Jumatatu jina la Roberto Lewandoski lilikuwepo kati ya majina 30 ya mwanzo ya wachezaji ambao wanagombania tuzo kubwa kabisa ya Ballon D’Or, Lewandoski jina lake limekuja baada ya msimu mzuri sana na Bayern Munich.
Ila hayo ni mambo ya kisoka, nje ya soka Roberto Lewandoski alikuwa na wakati mzuri sana kielimu, mshambuliaji huyu ametunukiwa degree yake ya kwanza ihusianayo na masuala ya elimu ya michezo.

0 comments:
Post a Comment