WAZIRI
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu amesema leo kuwa baada ya polisi
kufuatilia gari hiyo wamegundua iliyokuwa inamfuatilia Lissu ilikuwa na
namba batili huku gari halisi yenye namba hizo za usajili ikiwa Arusha.
“Utoaji wa taarifa na wenyewe haukuwa
rasmi kwa mfano Lissu aliposema kuna gari inamfuatilia nilielekeza
polisi wakaifuatilia ikakutwa Arusha kuna gari ndogo ya namba hizo kwa
hiyo kuna moja iliweka namba batili.
“Ile gari ilikutwa kule kule na haikuwa
na ruti ya huku (Dar es Salaam) huwa iko kule kule, kwa hiyo kwenye
mambo haya ndiyo maana tunahitaji sana ushirikiano.
“Natamani watu hawa tungewatia nguvuni
pale pale ningepewa ‘tip’ mapema tungefuatilia hili na kitendawili cha
watu wasiojulikana tungekitegua mara moja,” amesema Mwigulu akihojiwa na
Kituo cha Televisheni cha Clouds, leo.
Pamoja na mambo mengine amesema Lissu
mwenyewe anaweza kusaidia uchunguzi katika tukio hilo ambapo pia ameonya
watu watu wanaotengeneza matukio ya aina hiyo kufikiria madhara
yanayoweza kutokea baada ya tukio.
0 comments:
Post a Comment