Sunday, 24 September 2017

MSIGWA AUKWAA UGOMVI WA MSUKUMA NA RPC

Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA Peter Msigwa amezidi kushikilia suala la Mbuge wa Geita Mjini na RPC wa Geita na kusema kuna jambo kati yao lakini anashindwa kuelewa inakuaje mbaka sasa TAKUKURU inashindwa kuwahoji wote wawili.
Msigwa amesema hayo kupitia mtandao wake wa Twitter zikiwa zimepita siku kadhaa toka Mbunge na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita, Joseph Msukuma kudai kuwa ana siri nyingi za Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo na kudai atazitoa siri hizo ikiwa Kamanda wa Polisi huyo hatamuomba msamaha kwa kitendo alichomfanyia ikiwa pamoja na kumkamata na kumlaza rumande.

"Msukuma amesema anajua siri za RPC wa Geita , TAKUKURU kwa nini hamjiongezi kuwahoji wote wawili, kuna kitu hakipo sawa kinaendelea hapa" aliandika Mchungaji Msigwa
Mbunge wa Geita alikamatwa na jeshi la polisi na kulazwa rumande kwa masaa 24 kufuatia vurugu zilizofanywa katika mgodi wa Geita Gold Mine (GGM) lakini alipotoka Mbunge huyo alianza kumshtumu RPC wa Geita na kusema anafahamu mambo yake mengi, akahitaji kuombwa msamaha ndani ya siku tatu na RPC huyo huku akiahidi kutoa siri zake kama hatafanya hivyo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive