Mshambuliaji wa Everton, Wayne Rooney akivuja damu baada ya kuumia
kufuatia kugongana na Simon Francis wa Bournemouth katika mchezo wa Ligi
Kuu ya England leo Uwanja wa Goodison Park, lakini ajabu refa hakutoa
adhabu yoyote kiasi cha kuzomewa na mashabiki. Rooney alibadilishiwa
jezi baada ya kutibiwa na kuendelea na mchezo, Everton ikishinda 2-1
mabao yote yakifungwa na mshambuliaji Msenegali, El-Hadji Baye Oumar
Niasse dakika za 77 na 82 baada ya Joshua King kuanza kuwafungia wageni
dakika ya 49 .
0 comments:
Post a Comment