Dar es
Salaam. Bao la kipindi cha kwanza la Ibrahim Ajibu limeipa Yanga ushindi
wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda katika Uwanja wa Uhuru.
Kwa ushindi huo Yanga imefikisha pointi nane sawa na watani wao wa jadi Simba ambao Alhamisi walibanwa mbavu na Mbao kwa kulazimishwa sare ya mabao 2-2.
Timu zote hazikucheza vizuri na kujikuta wachezaji wao wakipatamiana na kusababisha baadhi yao kulimwa kadi za njano.
Wachezaji walioonyeshwa kadi za njano ni Papy Shishimbi na Raphael Daud kwa upande wa Yanga na Jabir Aziz alionyeshwa kadi ya njano kwa upande wa Ndanda.
Mashabiki wa Yanga waliondoka uwanjani kichwa chini kwa kuonyesha kutoridhishwa na mpira uliochezwa na timu yao.

0 comments:
Post a Comment