Showing posts with label BURUDANI. Show all posts
Showing posts with label BURUDANI. Show all posts

Wednesday, 7 February 2018

RIHANNA ATIKISA SENEGAL


Msanii maarufu duniani wa muziki wa Pop Robyn Rihanna Fenty maarufu kama Rihanna, amewasili nchini Senegal licha ya watu wa dini nchini humo kupinga ujio wake, wakimtuhumu kuwa ni mwanachama wa Iluminati (Freemason).

Akiwa nchini Senegal sambamba na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Rihanna ameshiriki kwenye kongamano kubwa la kuchangia kuinua sekta ya elimu nchini humo, na kusema kwamba hawataacha kufanya hivyo mpaka pale watakapohakikisha kila mtoto anakwenda shule na kupata elimu bora.

“Haya ni mapambano ambayo hatutaacha kwamwe kupambana mpaka pale kila mtoto wa kiume na mtoto wa kike ana uwezo wa kupata elimu”, alisikika Rihanna akisema hivyo.

Kwa upande wa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, amesema suala la kuchangia elimu sio la kujiamualia, ni suala nyeti na la loazima.

Kwenye mkutano huo uliofanyika Dakar nchini Senegal, Rihanna sambamba na Rais Emmanuel Macron wa Ufarsansa, waliwataka viongozi wa dunia na mashirika makubwa wanyotoa misaada kuongeza juhudi za kuinua elimu kwa nchi zinazoendelea barani Afrika.
Share:

Friday, 12 January 2018

MANENO YA MPOKI BAADA YA KUONA STUDIO ZA WCB

Mchekeshaji wa kundi la original comedy Mpoki ameamua kufanya utani kuhusiana na headquaters mpya za WCB baada ya kufanya vice versa na kile alichokipost Diamond Platnumz kwa kuonesha nyumba ya udongo katika page yake ya instagram na kusema ni studio za wachafu wakati Diamond alisema ni studio za wasafi.
Mpoki aliandika caption inayosema “tutaonana, hii ndio headquarters ya wachafu fm na tv kama kawa tukutane sehemu ya kuosha magari tutaonana hivi karibuni”
Share:

DIAMOND NA HARMONIZE WADHIHIRISHIA UMMA UJIO WA REDIO YAO

Baada ya kutuonesha mjengo mpya ambapo ndio zitakuwa ofisi za radio ya Wasafi FM na Wasafi Tv  sasa CEO wa WCB Diamond Platnumz  leo January 12, 2018 amepost picha inayomuonesha yuko na Harmonize huku nyuma yao kukiwa na mnara mrefu ambao inawezekana ukawa ndiyo mnara wa radio tuliyo ahidiwa..
Diamond amepost picha hiyo na kuandika Caption iliyosomeka…What a Busy Day #Mnarani…. InshaAllah Mwenyez Mungu atujaalie sisi Pamoja nawe Mwaka 2018 Uwe Mwaka Mwema na Wamafanikio…Tuseme “Ameen” Cc @harmonize_tz” – Diamond

Huwenda huu ukawa ndiyo mnara wa radio aliyoahidi kuileta kwa mashabiki wake na inategema kukamilika mwezi February mwaka huu 2018..
Share:

Friday, 6 October 2017

NGOZI ZA MASTAA HAWA ZAZUA UTATA

Jacqueline Wolper
BAADHI ya wasanii wamekuwa wakiwaacha wengi midomo wazi kutokana na mionekano yao ya sasa, wengi wao wakionekana kuwa na ngozi tofauti na walivyokuwa kipindi kifupi cha nyuma, wengine walikuwa weupe kiasi wamekuwa weupe zaidi pia wapo waliokuwa weusi sasa wamekuwa weupe.
Kwenye hili kuna mengi yamekuwa yakisemwa, ikiwemo kutumia vidonge vya kuwang’arisha ama mikorogo ya kisasa ya kupaka ambayo imezagaa inayotengenezwa na watu binafsi, ambayo inauzwa kwa bei ghari inayomtakatisha mtu bila kumgundua kirahisi kama humfahamu vyema.
Katika makala haya, wapo baadhi ya mastaa ambao ukiwaona zamani na sasa utagundua kuwa ngozi zao ni tata;
JACKLINE WOLPER
Kiuhalisia ni mweupe ila sasa kawa mweupe zaidi, jinsi alivyo huwezi kusema kwamba anajichubua ila muonekano wake unazua viulizo kwa mashabiki kwamba undani wa yeye kuwa hivyo ni upi, lakini msimamo wake ni kwamba hiyo ndiyo rangi yake na kinachochangia hivyo ni jinsi anavyojipenda na kuujali muonekano wake.
Staa wa filamu Bongo Yobnesh Yusuph ‘Batuli’
BATULI
Kiuhalisia bishosti huyu ni mweupe ila sasa amekuwa mweupe zaidi kutokana na masuala ya urembo unaochangiwa na vipodozi vya kisasa, naye ni miongoni mwa wasanii ambao mashabiki wake wamekuwa wakikosa majibu ya maswali yao.
TUNDA
Modo huyu naye ni mweupe kiasi, ila wengi wamekuwa wakimjaji muonekano wake wa kipindi cha nyuma na sasa, lakini mwenyewe hajali na wala hajawahi kueleza kwamba anatumia mikorogo ya kumbadilisha rangi yake ya asili.
HAMISA MOBETO
Bibie huyu amezua taflani kutokana na muonekano wake wengi wakimjaji kwamba awali alikuwa maji ya kunde lakini sasa kawa cheupe dawa na kujiuliza kulikoni bila swali hilo kupata jibu, sababu mwenyewe hayupo tayari kukiri hilo.
Amber Lulu
AMBER LULU
Amber naye anaingia katika listi hii ambaye bila kificho aliwahi kutokwa povu kuwa, hata kama anatumia mikorogo hakuna linayemuhusu hilo zaidi ya yeye na maamuzi yake sababu hakuna anayemsaidia kununua.
DAYNA
Awali wakati anaanza kutusua kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva alikuwa mweusi lakini siku hadi siku rangi yake imeonekana kubadilika na kuwa mweupe, ambapo aliwahi kukiri kujichubua kutokana na mambo ya ujana.
Kajala Masanja.
KAJALA
Mwanadada huyu kipindi cha nyuma alikuwa maji ya kunde lakini siku hadi siku rangi yake inabadilika kidogokidogo na sasa ameingia kwenye listi ya warembo weupe Bongo.
Vai wa Ukweli
Ni msanii wa filamu ambaye kipindi cha nyuma alikuwa mweupe kiasi lakini sasa amekuwa mweupe kama Mzungu.
SANDRA
Ni zao la Kundi la Kaole jina halisi ni Salma Salmini. Tangu kitambo alikuwa na weupe kidogo, lakini kadri siku zinavyozidi kuyoyoma amezidi kunga’ra na kuwa mweupe pee, jambo linalozua viulizo kwa mashabiki wake.
Share:

Monday, 4 September 2017

SHILOLE YAMKUTA MAZITO

Zuwena Mohamed ‘Shilole’.’
MKALI wa Bongo Fleva na Bongo Movies, Zuwena Mohamed ‘Shilole au Shishi Baby’ anadaiwa kubondwa na mpenzi wake wa sasa anayejulikana kwa jina moja la Uchebe, kisa kikisemekana ni wivu wa kimapenzi.
Chanzo makini kililiambia Ijumaa Wikienda kuwa, hivi karibuni Shishi alikwenda kwenye shoo mkoani Morogoro akiwa na Uchebe, akiwa jukwaani shabiki alipanda na kumshika kimahaba, alipomaliza shoo ndipo mchumba’ke huyo akamshushia kipigo.
Baada ya kuunyaka ubuyu huo, Ijumaa Wikienda lilimsaka Shishi ambaye alifunguka:
“Ni kweli kulitokea mgogoro wa kawaida, ilikuwa Zanzibar na siyo Morogoro. Unajua jamaa hatumii kilevi, sasa mimi nilimkwaza kwa sababu nilitaka kuendelea kunywa ndiyo tukapishana kauli. Kuhusu wivu ni kweli anao na huyu ni mwanaume nampenda sana siyo kama wengine waliopita,” alisema Shishi anayekimbiza na ngoma yake mpya ya Kigori.
Share:

Monday, 28 August 2017

ALICHOSEMA ALI KIBA BAADA YA KUWEKA HISTORIA

Alikiba.
Msanii wa muziki wa bongo fleva Alikiba ambaye amepewa cheo cha ‘Mfalme’ na mashabiki wake, amedhihirisha kuwa mashabiki hawakukosea kumpa cheo hicho, kwa kuvunja rekodi ya kutazamwa kwa video yake kwa mara nyingi zaidi ndani ya muda mfupi.
Kwenye ukurasa wake wa instagram, Alikiba ambaye siku ya Ijumaa ameachia video ya wimbo mpya ya ‘Seduce me’, ameweka post akiwashukuru mashabiki wake kwa kufanikisha kuvunja rekodi hiyo.
“Ahsanteni sana kwa upendo, nisingebarikiwa zaidi na kupendelewa bila nyinyi, nyinyi ni wa maana sana kwangu na nafanya haya kwa ajili yenu”, aliandika Alikiba.
Pamoja na hayo kwenye ukurasa wa instagram wa kampuni kubwa inayosimamia muziki wa Alikiba ya Rockstar. imeandika kuhusu rekodi ya video hiyo ambayo bado inaendelea kushika namba moja kweny video zinazotrend.
Historia ya kunjwa rekodi imewekwa, Mfalme Kiba na wimbo wake mpya waSeduce me umekuwa wa kwanza na kipee kwa msanii wa Afrika Mashariki kufikia kutazamwa mara milioni 1 kwenye Vevo/YouTube ndani ya masaa 38 tu, ina ‘trend’namba 1 Tanzania na namba 1 Kenya kwa ‘weekend’ nzima, rekodi imevunjwa”, iliandika Rockstar.
Share:

Saturday, 26 August 2017

SEDUCE ME YA KIBA YATIKISA

Staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’.
BAADA ya ukimya wa muda mrefu wa kutoachia ngoma mpya, staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ aliwaweka kwenye ‘kimuhemuhe’ mashabiki wake kwa kuonesha dalili za kuachia wimbo mpya ambao ulishakuwa maarufu kabla hata haujatoka.

Mkali huyu ambaye alikimbiza na wimbo wa Aje alioutoa mwaka jana, kwa kipindi chote hicho alikaa kimya na sasa ‘ameuvuruga’ ulimwengu wa burudani kwa ‘kubipu’ na posti zinazoashiria wimbo wake mpya uitwao Kipusa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram wenye mashabiki zaidi ya milioni mbili, Kiba alianza kutupia picha zilizoandikwa Kipusa na kuwafanya mashabiki wake wapagawe kwa kumtaka autoe wimbo huo haraka iwezekanavyo.

“I cant wait Kiba, achia bwana hiyo Kipusa iwakimbize wote wenye nyimbo mbovumbovu mjini,” aliandika mmoja wa wafuasi wa Instagram. KING NI KING Kiba ana historia ya kutoa wimbo au nyimbo kadhaa na zikakaa kwenye soko kwa muda mrefu tofauti hata na yule msanii anayejidai kuwa ni mpinzani wake wa jadi ambaye kila siku anatoa nyimbo lakini hazikai muda mrefu kwenye soko, zinaotea.

USHAHIDI NI HUU

Kabla ya Kiba hajatoa Chekecha Cheketua mwaka 2015, alikuwa kimya kwa muda mrefu lakini mashabiki wake waliendelea kusikiliza ngoma za kitambo kama Cindelera na Kidela. Alipoibuka mwaka huo, kila mmoja alikubaliana na ujio wake wa  Chekecha Cheketua kabla hajachagiza na Aje kisha Mwana. Hapo ndipo kila mtu alimjua Kiba ni nani. Kila mtaa, kila nyumba watu walisikika wakicheza nyimbo hizo za Kiba ambapo alidhihirisha ule usemi wake wa ‘nimepangusa kiti changu kilichokuwa na vumbi kisha nakikalia tena’.

UTOFAUTI WA KIBA

Tofauti na wasanii wengine, Kiba ni mwanamuziki. Namaanisha msingi wake umejengeka katika muziki. Anajua kuimba na vyombo, tofauti na wasanii wengi wa Bongo Fleva ambao ukiwaambia waimbe kwa vyombo, wataingia mitini.

HADI SASA HAKUPOA

Baada ya kuachia ngoma hizo, Kiba alikaa tena kimya hadi jana alipoaamua kuachia ngoma yake ya Kipusa (video na audio) na tayari imekuwa gumzo kila kona ya jiji.

SHOO KIBAO NJE YA NCHI

Kuonesha kwamba Kiba yupo vizuri, kwa wakati wote huo amekuwa akifanya shoo nyingi nje ya nchi.

AMEPIGA SHOO NEW YORK, MAREKANI

Huyo ndiye Kiba ambaye hata mwishoni mwa wiki iliyopita, aliandika historia kwa kufanya shoo matata sana pande za Marekani.

KOLABO KALI

Moja kati ya sifa nyingine kubwa ambayo Kiba anayo, amefanya kolabo nyingi sana ambazo kimsingi, hazijawaacha salama wenye nyimbo zao. Amefanya balaa kwenye kolabo kama Kiboko Yangu ya MwanaFA, amefunika mbaya katika Nisamehe ya Baraka The Prince na nyingine nyingi. Ana sauti kali ambayo anajua kuipangilia. Anapanda, anashuka.

Ni wasanii wachache sana wenye sifa ya namna hiyo duniani na ndiyo maana Kiba ameendelea kuwa Kiba miaka yote Bongo. Hata anayejiita mpinzani wake, anasifika kwa kutoa nyimbo nyingi ambazo mara nyingi zimegeuka kuwa kama big G lakini Kiba hata sasa akiimba Cindelera, bado mashabiki wataifurahia.
Share:

Friday, 18 August 2017

HILI NDIYO POVU ALILOTOA DIAMOND TWITTER

Baada ya Hamisa Mobetto kubadilisha jina la account ya mtoto wake kutoka Tanzanian Baby na kumuita Abdul Naseeb_Tz , twitter ya Diamond Platnumz imewaka moto kwa kauli kali ya SIMBA Inayotajwa kumlenga Mwanamke fulani anayetafuta Umaarufu.
Diamond ameandika “BITCH IS DYING FOR FAME!!!!!” 
#UshindiMediaNEWS
Share:

Tuesday, 15 August 2017

CHID BENZI AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA

Rapa Rashid Makwiro m,aarufu kama Chid Benz akipiga shoo hivi karibuni Uwanja wa Uhuru.
RAPA Rashid Makwiro maarufu kama Chid Benz na wenzake saba wamekamatwa na Jeshi la Polisi tangu Jumamosi baada ya kukutwa na dawa za kulevya maeneo ya Kariakoo jijini Dar, ikiwa ni siku chache baada ya kuhusishwa na tuhuma za matumizi ya madawa hayo.
Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba msanii huyo na wenzake wanaendelea kushikiliwa katika kituo cha polisi Msimbazi kwa mahojiano na upelelezi wa kina zaidi.
Soma habari Kamili Kesho katika Gazeti la Risasi Mchanganyiko.
Share:

WIMBO WA ROMA WAZUA MASWALI MENGI YASIYO NA MAJIBU


SIKU kadhaa baada ya kuanza kusambaa mitandaoni na kuchezwa kwenye vituo mbalimbali vya redio, wimbo wa Msanii wa Bongo Fleva, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’, umeibua maswali mengi.


Maswali yanaanzia kwenye jina la wimbo huo aliouita ‘Zimbabwe’, ambapo kwenye mashairi yake anasema ‘nakwenda Zimbabwe’, ambapo wengi wamejiuliza kwanini wimbo wa kuelezea kutekwa kwake aupe jina kama hilo.

Kwenye utambulisho wa wimbo huo katika moja ya kituo cha redio, msaani huyo aliwakilishwa na mkewe, Nancy Mshana, ambaye alisema mumewe ameshindwa kufika kwa sababu amesafiri kwenda Zimbabwe.

Mashairi mengine yaliyo kwenye wimbo huo ambayo yanaibua maswali ni pamoja na pale anaposema ‘na ripoti ya upelelezi vipi akiteka mtekaji?”

Anasema hayo wakati ambapo mpaka sasa, haijajulikana ni nani aliyemteka.

Katika wimbo huo aliouachia wiki hii sanjari na video yake, Roma ameeleza zaidi kuhusu maisha yake na namna alivyotekwa na watu wasiojulikana miezi michache iliyopita.

Huu ni wimbo wa kwanza kwa msaani huyo tangu kuibuka kwa taarifa za kutekwa kwake Aprili mwaka huu, na baadae kuonekana tana akiwa kwenye kituo cha polisi cha Oysterbay.

NANI ALIYEMTEKA?

Katika wimbo wake huo, alianza kuimba kwa kusema, “Wengi mlijiuliza aliyeniteka ni maaskari, mkanitafuta vituo vyote, Central hadi Sitakishari, wakasema hawajui nilipo.

“… mama alikwenda hadi mochwari… dah! Ya Kaisari, mwachie Kaisari. Machozi yenu yatalipwa mimi nafunga na kusali.”

Wimbo huo unaeleza pia,  namna ndugu, mashabiki na jamii kwa ujumla  walivyoguswa na kutekwa kwake na kwamba watalipwa na Mungu.

MATESO

Anasema angeweza kuwa tayari hata kufa kwa sababu ya harakati lakini kilichokuwa kikimuumiza zaidi ni familia yake.

“Mwanangu alimuuliza mama, baba lini atarudi? Na mke wangu aliwaliza, kuwashukuru sina budi… mimi siyo tu rapa ni baba wa familia na watoto nawapa mahitaji kama isemavyo Biblia…

“Kipi bora? Nife mseme nilikufa kiharakati, siogopi kufa ila nawaachaje wanaobaki? Je, nani kati yenu mwanangu atampa malezi, wapi atapata mahitaji, wapi atapata  mapenzi?

“Nilipokuwepo sikuwa najua hii saa nne, hii saa nane… nilichohitaji nitoke mzima na  ndugu zangu tuonane. Nimechapwa mijeledi, nimevunjwa bila huruma, asante mliopaza sauti, nimeiona nguvu ya umma.

“Siku tatu nimefungwa macho, mikono imefungwa nyuma… nakwenda Zimbabwe… yelele mamaaaaa.”

Aidha alitoa ufafanuzi kuhusu namna alivyotekwa ambapo alisema, ingawa inaelezwa kuwa alitekwa na watu waliomwingiza kwenye gari aina ya Toyota Noah, habari hizo si sahihi.

Alilaumu kitendo chake cha kutekwa akikiita kuwa ni cha uhuni wa kishamba huku akihoji waliomteka walikwenda wenyewe au kwa walitumwa.

Akizidi kuibua maswali katika wimbo huo, Roma alisema waliotabiri ataonekana kabla ya Jumapili, anawashukuru kwa vile utabiri wao ulitimia.

Roma alitekwa Aprili mwaka huu na kuzua maswali yaliyokosa majibu kuhusu nani aliyemteka na wapi alipokuwa.

Roma alitekwa akiwa na wenzake,  Monii Central Zone,  Bin Laden na Imma, ambaye ni mfanyakazi wa mama mzazi wa mmiliki wa studio za Tongwe Records iliyopo Masaki, Dar es Salaam, J Murder.

Ilidaiwa kuwa walivamiwa wakiwa studioni hapo majira ya saa 1:30 na kutekwa na watu wasiojulikana.
Share:

Monday, 24 July 2017

MBOTO: MZEE MAJUTO AJAFA



MSANII wa filamu nchini, Haji Salum maarufu kama Mboto, amekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zinazodai kuwa nguli wa Vichekesho katika tasnia ya uigizaji, Amri Athuman maarufu kama King Majuto amefariki dunia.
Mboto baada ya kupata taarifa hizi alifunga safari kuelekea mkoani Tanga ambapo ni nyumbani kwa Mzee Majuto na kumkuta hai, na amekanusha uvumi huo kupitia ukurasa wake wa Instagram  kwa kuposti picha inayowaonyesha yeye na Majuto  wakiwa nyumbani kwake, na picha hiyo iliambatana na maneno yafuatayo:
Baada ya kupata taarifa mbaya kuhusu Mzee Majuto nimelazimika kuja kwake Tanga. Ni kweli anaumwa ila anaendelea vizuri na si kama watu walivyozusha kuwa mzee hatunaye. Kwa sasa mzee ni mzima nipo naye Tanga,” ameandika Mboto.
Siku chache zilizopita, Ushindi Media ililiripoti taarifa za kuumwa kwa Mzee Majuto, anayesumbuliwa na tatizo la ngiri, lakini jana kwenye mitandao ya kijamii zikaenea taarifa zisizo za kweli kwamba King Majuto amefariki dunia.
Share:

Sunday, 23 July 2017

STAA WA FILAMU ZA HOME ALONE AFARIKI


 Mwigizaji John Heard aliyejizolea umaarufu kwa kuigiza kama baba katika filamu za Home Alone, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 72.



Mwili wake aligundulika na mhudumu wa hoteli aliyofikuwa amefikia kwa ajili ya mapumziko baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa mgongo jijini California, Marekani.

Heard alikuwa akiigiza kama Peter McCallister katika filamu za Home Alone akiwa baba wa Macaulay Culkin maarufu Kelvin.

Ameigiza katika filamu mbili kati ya hizo ambazo ni  Home Alone na Home Alone 2: Lost in New York
Share:

Saturday, 22 July 2017

CHINA YAMTOSA JUSTIN BIEBER


Justin Bieber.

Nyota wa muziki wa Pop duniani kutoka nchini Canada, Justin Bieber amepigwa marufuku kutumbuiza nchini China, kwa mujibu, katazo lililotolewa na Wizara ya Utamaduni nchini humo.
Taarifa ya wizara hiyo imeeleza kuwa haifai kwa watumbuizaji ambao wamejihusisha katika utovu wa nidhamu kuruhusiwa kuingia nchini humo.
Justin Bieber ni mwimbaji mwenye kipaji, lakini pia ni mwanamuziki kijana mwenye kuzua utata.
“Tunatumai kuwa, Justin Bieber atakapokomaa, anaweza kuendelea kuimarisha maneno yake na matendo, na kuwa mwanamuziki anayependwa kwa dhati na umma,taarifa hiyo imeeleza.
Justin Bieber akipozi.

Vyombo vya habari vimeeleza kuwa, China inaonekana sasa kumuweka Bieber katika orodha sawa na Dalai Lama na watu wanaopigania kujitenga kwa Taiwan.
Taarifa hizo zimetolewa baada ya wizara hiyo kujibu maswali kuhusu shabiki mmoja aliyeshangaa ni kwa nini hakuna ukumbi hata mmoja umetajwa kuwa utakuwa mwenyeji wa Bieber ilihali anatarajiwa kuanza ziara yake Barani Asia hivi karibuni.
Bieber aliwahi kuzuru China mwaka 2013, lakini sasa amejiunga na orodha ndefu ya wanamuziki waliopigwa marufuku kufanya shoo nchini humo.

Bieber na Serna Gomez.

Wengine ni bendi ya Uingereza kwa jina Oasis na kundi la Marekani kwa jina Maroon 5, ambao wamepigwa marufuku kwa sababu ya misimamo yao ya kisiasa badala ya tabia.
Mwaka 2014, Bieber, maarufu kwa wimbo wake Sorry alizua utata baada ya kuweka picha mitandaoni aliyopigwa akitembelea madhabahu ya Yasukuni jijini Tokyo.
Madhabahu hayo nchini Japan yalijengwa kwa heshima ya wanajeshi waliouawa vitani pamoja na wahalifu wa kivita lakini nchini China na Korea Kusini, hutazamwa kama ishara kwamba Japan haijajutia makosa yaliyotendwa na watawala wa nchi hiyzo miaka ya nyuma.
Share:

Friday, 21 July 2017

MAJUTO ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI


Baada ya kulazwa hospitali kwa muda wa siku tatu , muigizaji wa filamu za vichekesho Mzee Majuto ameruhusiwa na kurudi nyumbani kwake baada ya kufanyiwa upasuaji wa hernia (ngiri) mkoani Tanga.


Akizungumza kwa njia ya simu mke wa Mzee Majuto Bi. Aisha Majuto amesema kwamba tatizo lililokuwa likimsumbua mumewe lilianza siku nyingi ingawa  kwa wiki iliyopita hali ilibadilika na kuwa mbaya zaidi hadi kufikia kulazwa.

"Ni kweli tulikuwa tumelazwa lakini mume wangu amesharuhusiwa na kurudi nyumbani. Tatizo ni hernia (ngiri) na ameshafanyiwa upasuaji na anaendelea vizuri ingawa hawezi kuzungumza kwa muda mrefu", Bi Aisha Majuto.
Share:

Thursday, 20 July 2017

MAJUTO HALI MBAYA AOMBA DUA ZENU


Amri Athman ‘Mzee Majuto’ akiugulia.

MWEZI Mei, mwaka huu, gazeti ndugu la hili, Ijumaa Wikienda liliripoti habari mbaya juu ya lejendari wa vichekesho Bongo, Amri Athumani 'Mzee Majuto' kuwa katika hali mbaya kiafya, lakini kwa hali yake ilivyo kwa sasa anahitaji dua za Watanzania.

AFANYIWA UPASUAJI
Habari mbaya zilizolifikia Amani, mapema wiki hii zilieleza kuwa, Mzee Majuto yu kitandani kwa mara nyingine kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa uliosababisha afanyiwe upasuaji.
Chanzo makini kililieleza Amani kuwa, Mzee Majuto ambaye amezaliwa mwaka 1948, alilazwa kwa siku tano hospitalini huko mkoani Tanga akisumbuliwa na ugonjwa wa hernia (ngiri) ambapo ililazimu afanyiwe upasuaji ili kumsaidia kwenye tatizo lake hilo la muda mrefu.

Chanzo hicho kilieleza kuwa, kufuatia tatizo hilo, Mzee Majuto amekuwa akitumia dawa za hospitalini na zile za kienyeji, lakini hakuna unafuu wowote anaoupata.
“Kuna kipindi alilazwa hapo katikati, alipopata nafuu aliruhusiwa lakini wiki iliyopita alibanwa sana na unajua yule mzee alikuwa anaogopa kufanyiwa operesheni ila kutokana na afya yake imebidi akubali tu,” kilisema chanzo chetu hicho na kuongeza:
“Kimsingi Mzee Majuto anahitaji dua za mashabiki wake na Watanzania kwa jumla.”
Mzee Majuto.

MKE WA MZEE MAJUTO AFUNGUKA
Baada ya kupata habari hizo, Amani lilimtafuta msanii huyo kwa njia ya simu yake ya kiganjani ambapo ilipokelewa na mkewe, Aisha Yusuf ambaye alithibitisha mumewe kuumwa.

Mama Majuto alisema kuwa, hadi wakati anazungumza na gazeti hili alikuwa yupo na mumewe katika Hospitali ya Tanga Central Health Centre (TCHC) ambako alilazwa kwa siku tano na kufanyiwa upasuaji.
“Ni kweli Mzee Majuto anaumwa ndiyo maana nimepokea simu yake, nipo naye hapa hospitalini, anasumbuliwa na ugonjwa wa hernia ambao umeibuka na kumuanza tena.
“Tunamshukuru Mungu kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji hivyo Watanzania na mashabiki wake waendelee kumuombea na Mungu akipenda hivi karibuni tu atarudi mzigoni, watarajie mambo mazuri kutoka kwake,” alisema mama Majuto.

Amani lilipoomba kuzungumza na Mzee Majuto mwenyewe, mkewe alisema alikuwa usingizini kwani alitakiwa apumzike baada ya upasuaji.
“Nitamfikishia pole lakini haruhusiwi kuzungumza, anatakiwa kupumzika,” alisema mama huyo na kuongeza:
“Hata hivyo, tumeambiwa tutaruhusiwa kutoka hapa hospitalini muda wowote.”

MASHABIKI WAMMISS
Wakiongea na gazeti hili, baadhi ya mashabiki wa staa huyo walisema kuwa, wamemmiss sana kwenye fani yake ya uigizaji na kumuomba Mungu afanye miujiza na amrejeshee afya yake.
“Kwa kweli tumemmiss sana, tunaamini atapona na kurejea kwenye hali yake ya kawaida,” alisema mmoja wa mashabiki aliyejitambulisha kwa jina la Said Juma.
UGONJWA WA HERNIA
Hernia au ngiri ni aina ya ugonjwa ambao humpata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikilia au kubeba viungo (organs) fulani kupoteza uimara au kuwa na uwazi (opening) hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiliwa ipasavyo.

Miongoni mwa vitu vinavyoweza kumsababisha mtu kupata hernia ni pamoja na kuwa na uzito mkubwa au kuongezeka uzito kwa ghafla, kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu, ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua.
Pia kuharisha au kuvimbiwa (constipation). Vitu hivyo humfanya mtu apate hernia ambayo husababisha afanyiwe upasuaji ili kumaliza tatizo hilo.
CHANZO: AMANI
Share:

Tuesday, 18 July 2017

CHEMICAL,MTU KAMA NAY ANAWEZA KUWA HUBBY WANGU

Image result for msanii chemical




Msanii wa Bongo Flava Chemical ametaja sifa za mwanaume ambaye anamuhitaji katika maisha yake pindi atakapokuwa tayari kuingia katika mahusiano.


Ingawa rapper huyo ameeleza kwa sasa yupo single, amedai anampenda mwanamume ambaye si sharobaro na wakishakubaliana akajitambulishe nyumbani kwao.

“Mimi ni msichana fulani ambaye napenda mwanaume fulani lakini sijui, unajua mapenzi hayachagui, lakini mtu fulani ambaye ni nigger hard unajua sio sharobaro, kawaida real nigger kama Nay,” ameiambia Planet Bongo ya EA Radio na kuongeza.

“Mtu anayetaka aje kwenye familia afuate process, me am still traditional girl usione nafanya hip hop ukachukulia poa. Naamni kuna perfect guy wapo soma where, kwa aje afuate process then it will be ok,” amesisitiza Chemical.
Share:

Thursday, 6 July 2017

RASMI DIMPOZ KASAINI ROCKSTAR 4000 KUUNGANA NA KIBA



MKALI wa muziki, Ommy Dimpoz amesaini kufanya kazi na label kubwa ya muziki, RockStar4000 inayofanya kazi kwa ukaribu na kampuni kubwa ya muziki duniani, Sony Music Entertainment.
Muimbaji huyo kwa sasa ataungana na Ali Kiba ambaye alijiunga na label hiyo miaka 6 iliyopita, ambapo wiki iliyopita alitangazwa kuwa mmoja kati ya wamiliki wa label hiyo.


Ommy amefunguka haya kuhusu kujiunga kwake RockStar4000;
“Ni kweli nimesaini RockStar4000 kama ulivyosikia, kwahiyo kwa sasa nitakuwa nafanya kazi au kwa kifupi kazi zangu kuanzia sasa zitakuwa chini ya RockStar4000,” alisema Ommy Dimpoz.
“Nilikaa nao chini tukazunguma nikaona hili ni jambo zuri kwangu kwa sababu RockStar4000 ni kampuni kubwa duniani ambayo inafanya kazi za wasanii wengi sana. Kwahiyo PKP ikaona bora tufanye nao kazi ili kuupeleka muziki wa Ommy Dimpoz mbali zaidi.
“Kwahiyo mashabiki wakae mkao wa kula kwaajili ya Ommy mwingine ambaye atakuwa na sura nyingine kabisa,” aliongeza Ommy Dimpoz.
Pia label hiyo nchini Tanzania inafanya kazi na muimbaji Lady Jay Dee pamoja na Baraka The Prince.

Share:

Thursday, 29 June 2017

MZEE YUSUF ATANGAZA KUOA MKE MWINGINE



Image result for mzee yusuf



Zikiwa zimepita siku kumi tangu apate pigo la kufiwa na mkewe mdogo, Chiku Khamis, aliyekuwa Mfalme wa Taarab Bongo na Mkurugenzi wa Kundi la Jahazi Modern, Alhaj Mzee Yusuf kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu endapo ataoa mke mwingine.


Mzee Yusuf amefunguka alipoulizwa na Gazeti la Risasi endapo hali yake itarejea kama kawaida, Mzee Yusuf alisema kuwa suala hilo ni la Allah, hivyo akiamua aoe ataoa na kama ameamua kumpunguzia ili atulie, basi atatulia.

“Suala la kuoa tena ni la Allah, nitamuomba kama akiamua mimi nioe nitaoa, kama pengine amenipunguzia ili nitulie basi nitatulia maana hili jambo linatakiwa subira kwa kila kitu, hutakiwi kukurupuka, nikikurupuka nitajikuta nashindwa mtihani huu ambao Allah amenipa,” alisema Mzee Yusuf.

Mke wa Mzee Yusuf, Chiku alifariki Juni 17, mwaka huu katika Hospitali ya Amana alipokuwa akijifungua na kichanga chake na kuzikwa katika Makaburi ya Kisutu, Juni 18, akiwa ameacha watoto wawili wa kike.
Share:

Saturday, 24 June 2017

RAYVANNY ALETA TUZO NYUMBANI

By Brown Mgeni
June 24 2017
BET Viewer’s Choice Best New International Act
Hongera Kwa Msanii wa WCB Wasafi Rayvanny, Staa huyu wa Bongo Fleva ndio mshindi wa Tuzo ya BET Viewer’s Choice Best New International Act 2017
kwenye tuzo za #BETAwards2017. Rayvanny alikuwa akiwania tuzo hii na wasanii kutoka mataifa tofauti kama >>>
Best International Viewers Choice Awards Dave (UK) , Amanda Black (SA) , Changmo (South Korea), Rayvanny (Tanzania), Daniel Caesar, Remi, Skip Marley.




Share:

Friday, 23 June 2017

MUIGIZAJI ALIYEHITAJI KUMUUA TRUMP AINGIA MATATANI

NI UTANI WA NGUMI! Muigizaji mwenye jina kubwa Hollywood, Johnny Depp anaweza kuingia matatani baada ya kutoa utani jukwaani wa kumuua Rais wa Marekani, Donald Trump ili awe msanii wa pili kufanya hivyo nchini humo.

Staa huyo anayetamba na Muvi ya Pirates of Carribeans V iliyoingia sokoni mwezi huu aliingizia utani huo alipokuwa katika Tamasha la Glastonbury nchini Marekani kiasi kwamba alishangiliwa na umati wa watu uliokuwa mahali hapo.
“Nadhani anahitaji kusaidiwa!” alisema na kuongezea:
“Hivi mara ya mwisho ni lini kwa muigizaji kumuua rais wa Marekani?” aliuliza swali lililopokelewa kwa shangwe zaidi na watu waliokuwa mahali hapo.

Ikumbukwe tu kwamba mara ya mwisho kwa rais wa Marekani kuuliwa na muigizaji ilikuwa ni mwaka 1865 ambapo aliyekuwa rais, Abraham Lincoln aliuawa na jamaa anayeitwa John Wilkes Booth huku rais wa Marekani wa mwisho kuuawa na mtu wa kawaida alikuwa John F. Kennedy mwaka 1963.


Kwa utani huo, inawezekana Depp akaingia matatani kwa utani wake huo ambao ulionekana kuwafurahisha watu wengi waliokuwepo mahali hapo.
Share:

Ads

Blog Archive