Saturday, 22 July 2017

CHINA YAMTOSA JUSTIN BIEBER


Justin Bieber.

Nyota wa muziki wa Pop duniani kutoka nchini Canada, Justin Bieber amepigwa marufuku kutumbuiza nchini China, kwa mujibu, katazo lililotolewa na Wizara ya Utamaduni nchini humo.
Taarifa ya wizara hiyo imeeleza kuwa haifai kwa watumbuizaji ambao wamejihusisha katika utovu wa nidhamu kuruhusiwa kuingia nchini humo.
Justin Bieber ni mwimbaji mwenye kipaji, lakini pia ni mwanamuziki kijana mwenye kuzua utata.
“Tunatumai kuwa, Justin Bieber atakapokomaa, anaweza kuendelea kuimarisha maneno yake na matendo, na kuwa mwanamuziki anayependwa kwa dhati na umma,taarifa hiyo imeeleza.
Justin Bieber akipozi.

Vyombo vya habari vimeeleza kuwa, China inaonekana sasa kumuweka Bieber katika orodha sawa na Dalai Lama na watu wanaopigania kujitenga kwa Taiwan.
Taarifa hizo zimetolewa baada ya wizara hiyo kujibu maswali kuhusu shabiki mmoja aliyeshangaa ni kwa nini hakuna ukumbi hata mmoja umetajwa kuwa utakuwa mwenyeji wa Bieber ilihali anatarajiwa kuanza ziara yake Barani Asia hivi karibuni.
Bieber aliwahi kuzuru China mwaka 2013, lakini sasa amejiunga na orodha ndefu ya wanamuziki waliopigwa marufuku kufanya shoo nchini humo.

Bieber na Serna Gomez.

Wengine ni bendi ya Uingereza kwa jina Oasis na kundi la Marekani kwa jina Maroon 5, ambao wamepigwa marufuku kwa sababu ya misimamo yao ya kisiasa badala ya tabia.
Mwaka 2014, Bieber, maarufu kwa wimbo wake Sorry alizua utata baada ya kuweka picha mitandaoni aliyopigwa akitembelea madhabahu ya Yasukuni jijini Tokyo.
Madhabahu hayo nchini Japan yalijengwa kwa heshima ya wanajeshi waliouawa vitani pamoja na wahalifu wa kivita lakini nchini China na Korea Kusini, hutazamwa kama ishara kwamba Japan haijajutia makosa yaliyotendwa na watawala wa nchi hiyzo miaka ya nyuma.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive