Mshambuliaji wa Barcelona Neymar
mwenye umri wa miaka 25 amewaambia wachezaji wenzake kwamba atajiunga na
Paris St-Germain huku klabu hiyo ya Ufaransa ikitaka kumnunua nyota
huyo wa Brazil kwa kitita cha rekodi ya pauni milioni 196. (Le Parisen -
in French)
Lakini Meneja wa Barcelona Ernesto Valverde anasema
kuwa habari zinazomuhisisha Neymar na PSG ni uvumi na kwamba wanamtaka
kusalia (Metro)
Mchezaji mwenza Javier Mascherano bado anafikiri
kwamba klabu hiyo ya La liga inaweza kumzuia Neymar akisema kuwa ndio
tegemeo la klabu hiyo siku zijazo.(ESPN FC)
Barca inamlenga
mshambuiliaji wa Argentina Paulo Dybala mwenye umri wa miaka 23 kutoka
Juventus , iwapo Neymar ataondoka. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Manchester
City imekubali kumnunua beki wa kushoto Benjamini Mendy kutoka Monaco
kwa kitita cha pauni milioni 57(L'Equipe - in French)
Tayari PSG imejitayarisha kuwasilisha ombi la kitita cha pauni
milioni 70 kwa mshambuliaji wa Arsenal Alexi Sanchez mwenye umri wa
miaka 28 na kumlipa mshahara wa £ 400,000 kwa wiki.(Daily Mirror)
Manchester
United imewasilisha ombi la pauni milioni 35 kumnunua kiungo wa kati wa
Chelsea Nemanja Matic mwenye umri wa miaka 28 na wameambiwa kwamba
wanaweza kumchukua kwa pauni milioni 50 (Daily Mirror)
Real Madrid wamekubaliana na Monaco na Kylian Mbappe kuhusu uhamisho
utakaovunja rekodi ya pauni milioni 120 kumnunua mchezaji huyo mwenye
umri wa miaka 18. (Sun)
Barcelona imemuonya kiungo wa kati wa
Liverpool Phillipe Coutinho mwenye umri wa miaka 25 kwamba watamuandama
mshambuliaji wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele mwenye umri wa miaka
20 iwapo The Reds watakataa ombi lao. (Sun)
Arsenal wamepatiwa fursa ya kumsajili kiungo wa kati matata Rafinha mwenye umri wa miaka 24 kutoka Bercelona.(Sky Sports)
The Gunners pia wanakaribia kuingia mkataba na Crystal Palace ambao
utapelekea beki Calum Chambers kuelekea katika uwanja wa Selhurst
Park(Guardian)
Meneja wa Chelsea Antonio Conte anamtaka
mshambiliaji wa Swansea Fernando Llorente kuwa kama mchezaji wa ziada wa
Alvaro Morata lakini Swansea wanataka dau la pauni milioni 30
(Independent)
Mabingwa hao wa Uingereza pia wanamtaka kiungo wa
kati Alex Oxlaide-Chamberlain na wanapanga mazungumzo na mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 23.(Sky Sports)
Meneja Jurgen Klopp wa Liverpool anatarajiwa kumwambia kiungo wa kati
Phillipe Coutinho kwamba hawezi kuondoka Liverpool kuelekea Barcelona ,
baada ya The Reds kukataa kitita cha pauni milioni 72(Times -
subscription required)
Swansea ndio klabu ya hivi karibuni
inayohusishwa na uhamisho wa thamani ya pauni milioni 20 wa kiungo wa
kati wa Arsenal Jack Wilshere mwenye umri wa miaka 25(Daily Telegraph)
Meneja
wa Marseille Rudi Garcia amethibitisha kuwa mshambuliaji wa Arsenal
Olivier Giroud mwenye umri wa miaka 30 hatajiunga na klabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment