Aliyekuwa msemaji wa Klabu ya Yanga, Jerry Muro
amesema kuwa ilikufanikiwa katika utendaji ndani ya uongozi wa mabingwa
hao wa kihistoria ni lazima kuangalia ni nani anakuletea ushauri.
Muro ameyasema hayo ikiwa ni sikuchache
tu zimepita tangu Yanga imtangaze msemaji mpya wa timu hiyo, Dismass
Ten aliyochukua nafasi yake.
“Yanga kuna majungu watu wanapenda wafanye vitu vyao, kuna wanafiki ambao watakwambia ufanye hiki ukikifanya unaingia chaka.
“Wapo Yanga SC watu wenye msaada wa kweli, wazuri sana, wenye akili na wenye mapenzi ya kweli kuhakikisha Yanga inakuwa kama TP Mazembe watu wote hao wapo Yanga.
“Unachotakiwa kufanya ni kufungua macho
kuangalia ni nani anakuletea ushauri, maana kuna mwingine anakuletea
ushauri wakati yeye kashindwa kuongoza nyumba yake kaachana na mkewe
,hajali watoto wake yeye mwenyewe kufua nguo hafui nguo maisha yake
yamemshinda,” alisema Jerry Muro aliyekuwa msemaji wa klabu hiyo.
Mungu anasema unapojipenda nafsi yako
wewe mpende na jirani, kaka kama MTU kashindwa kuendesha familia yake
kamwe hawezi kuendesha Yanga”. Muro ameyasema hayo kupitia chombo cha
habari cha UFM radio.
0 comments:
Post a Comment