MKALI wa Bongo Fleva na Bongo Movies,
Zuwena Mohamed ‘Shilole au Shishi Baby’ anadaiwa kubondwa na mpenzi wake
wa sasa anayejulikana kwa jina moja la Uchebe, kisa kikisemekana ni
wivu wa kimapenzi.
Chanzo makini kililiambia Ijumaa Wikienda kuwa,
hivi karibuni Shishi alikwenda kwenye shoo mkoani Morogoro akiwa na
Uchebe, akiwa jukwaani shabiki alipanda na kumshika kimahaba,
alipomaliza shoo ndipo mchumba’ke huyo akamshushia kipigo.
Baada ya kuunyaka ubuyu huo, Ijumaa Wikienda lilimsaka Shishi ambaye alifunguka:
“Ni kweli kulitokea mgogoro wa kawaida,
ilikuwa Zanzibar na siyo Morogoro. Unajua jamaa hatumii kilevi, sasa
mimi nilimkwaza kwa sababu nilitaka kuendelea kunywa ndiyo tukapishana
kauli. Kuhusu wivu ni kweli anao na huyu ni mwanaume nampenda sana siyo
kama wengine waliopita,” alisema Shishi anayekimbiza na ngoma yake mpya
ya Kigori.
0 comments:
Post a Comment