WASHAMBULIAJI wa kutumainiwa wa Yanga, Obery Chirwa pamoja na Amissi Tambwe
leo hii wataungana na kikosi hicho katika mazoezi ya kujiandaa na mechi
yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Njombe Mji katika Uwanja wa Uhuru jijini
Dar es Salaam.
Yanga na Njombe Mji zitapambana
Jumamosi hii katika Uwanja wa Sabasaba mijini Njombe baada ya Shirikisho
la Soka Tanzania kuifanyia mabadiliko ratiba ya ligi kuu ambapo awali
ilikuwa zipambane Jumatano hii.
Kitendo hicho cha nyota hao kujiunga na
kikosi hicho kimepokelewa kwa mikono miwili na viongozi wa benchi la
ufundi la timu hiyo baada ya kuwakosa kwa kipindi kirefu kutokana na
kusumbuliwa na majeraha ya goti.
Majeraha hayo yaliwafanya wawe nje ya
uwanja kwa kipindi kirefu huku wakishindwa kuitumikia timu yao hiyo
katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba lakini pia ule wa Ligi Kuu
Bara dhidi ya Lipuli FC. Mechi zote hizo Yanga haikufanya vizuri.
Akizungumza na Championi Jumatatu,
Daktari wa Yanga, Edward Bavu, alisema kuwa wachezaji hao kwa pamoja leo
hii wataanza mazoezi baada ya kupona majeraha yao.
“Hakika tunamshukuru Mungu kwa hilo kwani wamerejea katika kipindi muafaka baada ya kupona majeraha yao ya goti.
“Kwa hiyo, mpaka kufikia hapa kazi
iliyobakia ni kwa makocha kuhakikisha wanawapatia mazoezi ya ufiti kabla
ya kuanza kuwatumia katika mechi zijazo,” alisema Bavu na kuongeza:
“Wachezaji ambao tutaendelea kuwakosa
kikosini kwetu ni kipa Beno Kakolanya na Geofrey Mwashiuya ambao wote
bado ni majeruhi na wanaendelea na matibabu.”
0 comments:
Post a Comment