BAADHI ya wasanii wamekuwa wakiwaacha wengi midomo wazi kutokana na
mionekano yao ya sasa, wengi wao wakionekana kuwa na ngozi tofauti na
walivyokuwa kipindi kifupi cha nyuma, wengine walikuwa weupe kiasi
wamekuwa weupe zaidi pia wapo waliokuwa weusi sasa wamekuwa weupe.
Kwenye hili kuna mengi yamekuwa yakisemwa, ikiwemo kutumia vidonge
vya kuwang’arisha ama mikorogo ya kisasa ya kupaka ambayo imezagaa
inayotengenezwa na watu binafsi, ambayo inauzwa kwa bei ghari
inayomtakatisha mtu bila kumgundua kirahisi kama humfahamu vyema.
Katika makala haya, wapo baadhi ya mastaa ambao ukiwaona zamani na sasa utagundua kuwa ngozi zao ni tata;
JACKLINE WOLPER
Kiuhalisia ni mweupe ila sasa kawa mweupe zaidi, jinsi alivyo huwezi
kusema kwamba anajichubua ila muonekano wake unazua viulizo kwa
mashabiki kwamba undani wa yeye kuwa hivyo ni upi, lakini msimamo wake
ni kwamba hiyo ndiyo rangi yake na kinachochangia hivyo ni jinsi
anavyojipenda na kuujali muonekano wake.
BATULI
Kiuhalisia bishosti huyu ni mweupe ila sasa amekuwa mweupe zaidi
kutokana na masuala ya urembo unaochangiwa na vipodozi vya kisasa, naye
ni miongoni mwa wasanii ambao mashabiki wake wamekuwa wakikosa majibu ya
maswali yao.
TUNDA
Modo huyu naye ni mweupe kiasi, ila wengi wamekuwa wakimjaji
muonekano wake wa kipindi cha nyuma na sasa, lakini mwenyewe hajali na
wala hajawahi kueleza kwamba anatumia mikorogo ya kumbadilisha rangi
yake ya asili.
HAMISA MOBETO
Bibie huyu amezua taflani kutokana na muonekano wake wengi wakimjaji
kwamba awali alikuwa maji ya kunde lakini sasa kawa cheupe dawa na
kujiuliza kulikoni bila swali hilo kupata jibu, sababu mwenyewe hayupo
tayari kukiri hilo.
AMBER LULU
Amber naye anaingia katika listi hii ambaye bila kificho aliwahi
kutokwa povu kuwa, hata kama anatumia mikorogo hakuna linayemuhusu hilo
zaidi ya yeye na maamuzi yake sababu hakuna anayemsaidia kununua.
DAYNA
Awali wakati anaanza kutusua kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva
alikuwa mweusi lakini siku hadi siku rangi yake imeonekana kubadilika na
kuwa mweupe, ambapo aliwahi kukiri kujichubua kutokana na mambo ya
ujana.
KAJALA
Mwanadada huyu kipindi cha nyuma alikuwa maji ya kunde lakini siku
hadi siku rangi yake inabadilika kidogokidogo na sasa ameingia kwenye
listi ya warembo weupe Bongo.
Vai wa Ukweli
Ni msanii wa filamu ambaye kipindi cha nyuma alikuwa mweupe kiasi lakini sasa amekuwa mweupe kama Mzungu.
SANDRA
Ni zao la Kundi la Kaole jina halisi ni Salma Salmini. Tangu kitambo
alikuwa na weupe kidogo, lakini kadri siku zinavyozidi kuyoyoma amezidi
kunga’ra na kuwa mweupe pee, jambo linalozua viulizo kwa mashabiki wake.
0 comments:
Post a Comment