Msanii wa muziki wa bongo fleva Alikiba ambaye amepewa cheo cha ‘Mfalme’
na mashabiki wake, amedhihirisha kuwa mashabiki hawakukosea kumpa cheo
hicho, kwa kuvunja rekodi ya kutazamwa kwa video yake kwa mara nyingi
zaidi ndani ya muda mfupi.
Kwenye ukurasa wake wa instagram,
Alikiba ambaye siku ya Ijumaa ameachia video ya wimbo mpya ya ‘Seduce
me’, ameweka post akiwashukuru mashabiki wake kwa kufanikisha kuvunja
rekodi hiyo.
“Ahsanteni sana kwa upendo, nisingebarikiwa zaidi na kupendelewa bila
nyinyi, nyinyi ni wa maana sana kwangu na nafanya haya kwa ajili yenu”, aliandika Alikiba.
Pamoja na hayo kwenye ukurasa wa
instagram wa kampuni kubwa inayosimamia muziki wa Alikiba ya Rockstar.
imeandika kuhusu rekodi ya video hiyo ambayo bado inaendelea kushika
namba moja kweny video zinazotrend.
Historia ya kunjwa rekodi imewekwa, Mfalme Kiba na wimbo wake mpya wa ‘Seduce me‘
umekuwa wa kwanza na kipee kwa msanii wa Afrika Mashariki kufikia
kutazamwa mara milioni 1 kwenye Vevo/YouTube ndani ya masaa 38 tu, ina
‘trend’namba 1 Tanzania na namba 1 Kenya kwa ‘weekend’ nzima, rekodi
imevunjwa”, iliandika Rockstar.
0 comments:
Post a Comment