Beki mpya wa Simba, Erasto Nyoni ameanza kufuata nyayo za beki
mwingine wa timu hiyo, Shomari Kapombe katika kutupia mabao.
Kapombe ndiye beki alifunga mabao mengi katika miaka ya karibuni ambapo alifunga mabao manane Ligi Kuu msimu wa 2015/16.
Hata
hivyo Nyoni ambaye ametua Simba msimu huu, ameanza kuweka rekodi ya
aina yake baada ya kufunga mabao manne katika mechi nane alizocheza hivi
karibuni.
Nyoni alianza kwa kufunga bao safi kwenye
mchezo wa Taifa Stars na Zambia katika michuano ya COSAFA kabla ya
kufunga tena katika mchezo wa kirafiki kati ya Bidvest Wits ya Afrika
Kusini na Simba.
Beki huyo anayemudu kucheza nafasi
zote za ulinzi, alifunga pia dhidi ya Gulioni ya Zanzibar kabla ya
kufunga tena dhidi ya Ruvu Shooting juzi Jumamosi hivyo kuwa beki wa
Simba aliyecheka na nyavu
0 comments:
Post a Comment