Monday, 14 August 2017

CRISTIANO RONALDO AFUNGIWA

Mchezaji Cristiano Ronaldo akibishana na refa katika mechi ya jana.
Staa wa soka wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amerudi kwenye headlines baada ya chama cha soka cha Hispania kufikia maamuzi ya kumfungia jumla ya mechi 5 kucheza kwa kosa la kumsukuma refa wa game ya El Clasico Real Madrid dhidi ya Barcelona katika game iliyochezwa Nou Camp.
Cristiano Ronando amefungiwa game hizo tano baada ya kumsukuma refa Ricardo de Burgos wa game ya El Clasico, ambaye alimuonesha kadi ya pili ya njano dakika ya 82 baada ya Ronaldo kujiangusha katika eneo la 18 la FC Barcelona kitendo kinatafsirika kuwa amedanganya, Ronaldo mechi nne amefungiwa kwa kosa la kumsukuma refa na moja kutumikia kadi nyekundu.
Baada ya kupewa adhabu hiyo Cristiano Ronaldo ataukosa mchezo wa marudiano dhidi ya Barcelona usiku wa August 16 na game nne za ufunguzi wa LaLiga ambazo dhidi ya Deportivo La Coruna August 20, Valencia August 27, Levante September 10 na Real Sociedad September 17.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive