Monday, 14 August 2017

DONDOO ZA SOKA ULAYA JUMATATU 14.08.2017

Ivan Perisic (kulia) alikuwa anachezea Wolfsburg kabla ya kujiunga na Inter Milan
Chelsea wanafikiria kutaka kumsajili mchezaji anayenyatiwa na Manchester United Ivan Perisic, 28, kutoka Inter Milan. (Mirror)

Barcelona wanataka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 26. (Diario Gol)
Cezar Azpilicueta, 27, anadhani Chelsea wanahitaji kusajili wachezaji kadhaa zaidi kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Evening Standard)
Chelsea wapo tayari kupanda dau la pauni milioni 50 wiki hii kumtaka beki wa kati wa Southampton Virgil van Dijk na kuwapiku Liverpool. (Daily Star)
Manchester United watakuwa tayari kulipa pauni milioni 36.5 kumsajili kiungo wa Barcelona Sergi Roberto, 25, ikiwa mchezaji huyo atataka kuondoka Uhispania. (Don Balon)
Manchester United wanakaribia kufikia makubaliano na Oliveirense ya Ureno kumsajili mshambuliaji Bruno Amorim, 19. (Daily Mail)
Antoinne Griezmann, 26, atachukizwa na hatua ya Atletico Madrid kumuuza kipa wake Jan Oblak na huenda akafikiria kuhamia Manchester United. (Don Ballon)
Leicester City watakataa dau la Roma la pauni milioni 31 la kumtaka Rirad Mahrez. Leicester wanataka pauni milioni 50. (Mirror)
Virgil van Dijk amechezea Uholanzi mechi 12
Mkurugenzi mkuu wa Juventus Beppe Marotta amesema wanamtaka kiungo anayesakwa na Liverpool Naby Keita, 22, anayechezea RB Leipzig. (La Gazzetta dello Sport)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema anahitaji kuimarisha kikosi chake kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Liverpool Echo)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anafikiria kumsajili mshambuliaji wa Napoli Lorenzo Insigne, kuchukua nafasi ya Philippe Coutinho anayenyatiwa na Barcelona. (Express)
Barcelona hawatokata tamaa ya kumsajili Philippe Coutinho, 25, kutoka Liverpool, na wapo tayari kutoa pauni milioni 137 kumshawishi mchezaji huyo. (The Sun)
Mshambuliaji wa Real Madrid Marco Asensio atakuwa na mazungumzo ya dharura na klabu yake kuhusiana na kutaka kuhamia Arsenal. (The Mirror)
Tottenham wataongeza bidii ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Lazio Keita Balde, 22, ambaye hakupangwa katika kikosi cha kwanza kwenye mechi iliyopita. (Mirror)
Baba Rahman
Winga wa PSG Jese Rodriguez, 24, amekataa kwenda Fiorentina kwa mkopo na anajiandaa kwenda Stoke kwa mkopo. (Sun)
Schalke wanazungumza na Chelsea kuhusu kumchukua tena kwa mkopo beki Baba Rahman, 23. (Sky Sports)
Newcastle wameongeza bidii ya kujaribu kumsajili kiungo wa Arsenal Jack Wilshere, 25, baada ya mchezaji huyo kuachwa katika kikosi kilichocheza dhidi ya Leicester. (Sun)
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na wiki njema.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive