Nadhani leo yaweza kuwa ni siku bora zaidi kwa raisi wa Marekani Donald Trump kwani leo ndiyo siku pekee ambayo rais huyo amepata nafasi ya kukaa meza moja na rais wa Urusi Vladimir Putin.
Trump amekutana na rais huyo wa Urusi katika mkutano wa nchi zenye uchumi mkubwa alimaarufu G20 Hamburg, nchini Ujerumani.
Mkutano huo umaeanza siku ya leo na kuhuzuriwa na marais, mawaziri pamoja na wawakilishi wa nchi husika.
Rais Trump alionekana kufurahia sana kuonana na Putin kiasi cha kusema kuwa ni neema kukutana na wewe.
Ikumbukwe kuwa nchi hizo mbili ziko katika vita baridi lakini leo wameamua kukaa meza moja na kufanya mazungumzo ya kina.
Katika mazungumzo hayo Rais Trump aliongozana na katibu wake Rex Tillerson pamoja na mkalimani huku Putin nae akiongozana na waziri wake wa mambo ya nje Sergey Lavroy pamoja na mkalimani wao.
kwa muujibu wa Dailmail lengo la mazungumzo hayo ya marais hayo ikiwa ni agenda ya Ukraine na majeshi ya Nato.
lakini taarifa kutoka ndani ya ikulu ya Marekani zinadai kuwa mazungumzo baina ya mafahari hayo yalenga kuweka ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
Good
ReplyDelete