Sahihi kusema Mwenyezi Mungu ni mkubwa na kila nafsi itaonja mauti.
Habari si njema katika familia ya soka ya England na duniani kote, nayo ni kifo cha mtoto Bradley Lowery.
Bradley shabiki namba moja wa Sunderland na rafiki namba moja wa mshambulizi mkongwe wa Sunderland na England, Jermain Defoe.
Mtoto
huyo aliyekuwa amefikisha miaka sita alianza kupambana na ugonjwa wa
kansa tokea mwaka 2013 na alikuwa maarufu baada ya urafiki wake kusikika
kila sehemu.
Mwenyezi Mungu amrehemu.
Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi amina.
ReplyDelete