Mambo mengi yanaendelea hivi sasa lakini kubwa mojawapo ni
kwamba baada ya bata refu la likizo sasa wachezajj wa Ulata wanarudi
vilabuni mwao kuanza maandalizi ya msimu ujao wa ligi.
Wachezaji wa Manchester United nao wameanza kurudi kujianda na safari
ya kwenda Marekani na timu yao na waliorudi tayari walifanyiwa hadi
photoshoot ya jezi mpya kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.
Henrikh Mkhitaryan ni mmoja kati ya waliorudi na ukifungua ukurasa wa
Instagram wa Manchester United naye utaona ni kati ya wachezaji
waliopiga picha wakiwa na jezi mpya ya klabu hiyo.
Lakini usichokijua ni kwamba kuna picha ya Mkhitaryan ambayo nayo
ilipaswa kutangaza jezi hizo lakini imeondolewa katika orodha ya picha
ambazo zitatumika kutangaza uzi huo mpya wa United.
Picha hiyo mwanzo United waliipost katika kurasa zao na ikaondolewa
kwa sababu ya muonekano wa Mualmernia huyo ambaye anaonekana wazi
alikula bata la kupitiliza wakati wa likizo.
Mkhitaryan anaonekana kuanza kutoka kitambi na kunenepa suala ambalo
United wameona sio vyema kulionesha sana, na ili kulinda image ya
mchezaji huyo ndio maana Manchester wakaamua kuiondoa picha hiyo.
0 comments:
Post a Comment