Friday, 7 July 2017

TETESI ZA SOKA ULAYA IJUMAA 7/7/2017 NA DENIS MASSAWE

Mustakabali wa meneja wa Chelsea, Antonio Conte uko mashakani baada ya meneja huyo kukasirishwa na shughuli nzima ya usajili katika klabu hiyo (Daily Mirror).
Hatua ya Manchester United kutaka kumsajili Romelu Lukaku, 24, haihusiani na mkataba ambao utamrejesha Wayne Rooney, 31, Everton (Liverpool Echo).
Chelsea bado wanatarajiwa kujaribu kumsajili Romelu Lukaku, 24, licha ya taarifa kuwa mchezaji huyo amekubali kuhamia Manchester United kwa pauni milioni 75 kutoka Everton (Guardian).
Mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, 24, ameachwa "kwenye mataa" baada ya Manchester United kumsajili Romelu Lukaku. Morata alikuwa na uhakika kuwa anahamia Old Trafford (Independent).
Romelu Lukaku amekubali kusaini mkataba wa muda mrefu Manchester United na mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki (Daily Star).
Chelsea huenda wakakabiliwa na tatizo la mshambuliaji baada ya Diego Costa kuanza kuaga wachezaji wenzake kufuatia kuambiwa na Antonio Conte kuwa hayuko kwenye mipango yake msimu ujao (Daily Telegraph).
Chelsea wanajiandaa kutoa dau "kubwa" kumtaka kiungo wa Real Madrid James Rodriguez (AS).
Chelsea sasa wameelekeza macho yao kwa mshambuliaji wa Swansea Fernando Llorente, 32, baada ya kushindwa kumpata kwa mkopo mwezi Januari (Evening Standard)




Barcelona wamekasirishwa na nahodha wao wa zamani Carles Puyol, baada ya mchezaji anayemwakilisha Eric Garcia, 16, kuamua kuhamia Manchester City (Independent).
Everton wanajiandaa kupanda dau jipya la pauni milioni 32 kumtaka kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 27 (Daily Mail).
Kipa wa Stoke City Jack Butland, 24, amesema anaweza 'kufikiria' iwapo Manchester United watamtaka (Manchester Evening News).



Arsenal wanamtaka kiungo wa Eintracht Frankfurt Aymen Barkok, 19 (Spox).
Marseille wanaongoza katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 30, kwa kitita cha pauni milioni 24.7, baada ya Arsenal kufanikisha usajili wa Alexandre Lacazette (Daily Telegraph).
Arsenal hawataki kulipa kiasi ambacho Leicester wanakitaka ili kumsajili winga Riyad Mahrez, 26, ambaye anatarajiwa kuondoka Leicester msimu huu (Daily Star).
Barcelona wapo tayari kutoa pauni milioni 26 kumsajili beki wa Arsenal Hector Bellerin (Sport).
Arsenal wanamfuatilia kiungo wa Monaco Fabinho (France Football).
Winga wa zamani wa Newcastle Hatem Ben Arfa, 30, ameambiwa anaweza kuondoka Paris Saint-Germain (L'Equipe).
Paris Saint-Germain watamgeukia Philippe Coutinho iwapo watashindwa kumsajili Kylian Mbappe kutoka Monaco. PSG wapo tayari kutoa pauni milioni 70 kumchukua Coutinho (Le10sport).
Winga Demarai Gray, 21, anataka kuhakikishiwa namba Leicester huku Tottenham na Liverpool zikimnyatia (Daily Mirror).
Dau la pauni milioni 22 la Barcelona kumtaka kiungo wa zamani wa Tottenham, Paulinho, 28, limekataliwa na klabu yake ya Guangzhou Evergrande (Sky Sports).



Licha ya Guangzhou Evergrande kukataa, Barcelona watarejea na dau jingine kumtaka Paulinho (Cadena SER).
Stoke City wamekuwa na mazungumzo na Manchester City ya kumsajili kiungo Fabien Delph, 27 (Stoke Sentinel).
Real Madrid wamekuwa na mazungumzo ya siri na PSG kuhusu Marco Verratti,24 (Don Balon).
Real Madrid wamekuwa na mazungumzo mapya na Kylian Mbappe (Marca).
Real Madrid watakuwa tayari kumruhusu Gareth Bale kuondoka kwa pauni milioni 88 (Diario Gol).
Watford wanazungumza na Chelsea kuhusu kiungo Nathaniel Chalobah, 22, na wana uhakika mchezaji huyo anataka kurejea Vicarage Road (London Evening Standard).



Aston Villa wamemuulizia kipa wa Manchester City Joe Hart (Birmingham Mail).
AC Milan sasa wamemgeukia mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang, 28, na pia wanamtaka Nikola Kalinic (Gianluca Di Marzio).
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa.
Share:

1 comment:

  1. Da yaani kila day lazima nitembelee hii blog ili nicheki tetesi za soka maani wewe jamaa ujawahi muacha mtu salama.

    ReplyDelete

Ads

Blog Archive