Sunday, 15 January 2017

PICHA 20: MAGEREZA AMBAYO YAMEGEUZWA KUWA MAJUMBA YA KIFAHARI


Kubadilisha matumizi ya majengo mbalimbali imekuwa ni kawaida kwa nchi mbalimbali, watu wameendelea kufikiria namna ya kubadilisha matumizi ya majengo mbalimbali ili kufanya biashara zaidi.
Leo January 15 2017 nimekutana na haya majengo kutoka sehemu mbalimbali duniani ambayo yalibadilishwa matumizi yake na kuboreshwa zaidi kutoka kuwa magereza na kuwa sehemu kama vile shule na Hoteli.
Gereza la Pentrige, Melbourne Australia 
Hili lilikuwa ni gereza lakini mtu binafsi alinunua eneo hili mwaka 2013 na kubadilisha kuwa makazi ya watu na hotel ya kifahari
Centro Civico, Palencia Spain 
Hispania ilibadilisha gereza hili na kuwa kituo cha utamaduni na sanaa
Convent of the Penitents, Ufaransa
Gereza hili lilibadilishwa na kuwa shule ya muziki
Four Seasons Hotel, Instabul Uturuki
Hii ni hoteli lakini lengo la msingi la kujengwa kwake ilikuwa ni kuwa gereza
Hullet House, Hong Kong
Jengo hili lilijengwa mwaka 1881 na lilikuwa likitumika kama makao makuu ya gereza la askari wa majini
Gereza la Reading, Uingereza
Wageni wengi wamefika gereza la Reading Uingereza, baada ya kufunguliwa kwa mara ya kwanza ajili ya umma September 2016 kama nafasi ya maonyesho.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive