By Denis Massawe
Leo
December 30, 2016 Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini (TPBC) imetangaza
kumfungia kwa miaka miwili Bondia wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka
kufuatia kitendo chake cha kugoma kupanda ulingoni kupigana na Bondia
Abdallah Pazi “Dullah Mbabe”.
Pambano
hilo ilikuwa lifanyike Desemba 25 mwaka huu, katika Ukumbi wa PTA Saba
saba jijini Dar es salaam, lililoandaliwa na Promota Siraju Kaike
kupitia kampuni yake ya Kaike Promotion.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Katibu
Msaidizi wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini (TPBC), Chatta Michael
amesema kuwa Kamisheni yake ilitoa kibali cha kufanyika kwa mpambano huo
baada ya kujiridhisha kuwa taratibu zote zimefuatwa na mabondia
wameridhia na kukubaliana na muandaaji, Ila wameshangwaza na Bondia
Francis Cheka kugoma kupanda ulingoni kwa madai ya malipo
wakati alishasaini mkataba na muandaaji ulioonyesha kuwa ameshachukua
kiasi cha shilingi milioni tatu (3,000,000) na baada ya mpambano
alitakiwa kupewa kitita chake cha milioni sita.
Amesema
kitendo kilichofanywa na Cheka kinaweza kupoteza uaminifu baina ya
mabondia na waandaaji wa mapambano, kujiondoa kwa waandaaji katika
mchezo huo kwa kuona hakuna uaminifu na pia kinaweza sababisha uvunjifu
wa amani kwa watazamaji, iwapo wataendelea kudanganywa uwepo
wa mapambano hewa.
Hivyo
Kamati ya utendaji ya Kamisheni hiyo iliyokaa Desemba 27, na kupitia
kanuni za mchezo huo, imemkuta Bondia Francis Cheka na makosa
ya kimakubaliano na kutangaza kumfungia kujihusisha kwa namna yeyote
na mchezo huo na kutakiwa kulipa faini ya shilingi laki tano (500,000).
0 comments:
Post a Comment