Saturday, 21 January 2017

HAYA NDIO MANENO MISS TZ 2004 FARAJA NYALANDU KUHUSU MKE WA TRUMP


Miss Tanzania 2004 Faraja Nyalandu ambaye ni mke wa zamani wa Waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu ni miongoni mwa waliofatilia kwa karibu kuanzia uchaguzi wa Urais Marekani ambapo baada ya Trump kuapishwa jana ameyaandika yafuatayo.
"Mwaka 1996 Melania Knavs akiwa na miaka 26 aliingia Marekani akiwa na ndoto ya kuwa mwanamitindo, jana,akiwa ni Melania Trump, alishika Biblia aliyotumia kuapa Rais wa 45 wa Marekani, Rais Donald Trump."
"Ukiniuliza kama alidhani kuna siku angesimama Capitol Hill kwenye uapisho wa Rais kama Mke wa Rais wa Marekani, nitakwambia hapana….. lakini ndivyo Mungu alivyo."
Faraja
"Leo hii huitaji kumheshimu Melania Trump ila utaheshimu mamlaka yake, na kwakuwa amekalia hicho kiti chenye mamlaka, utajikuta unamheshimu tu, unaweza kudhihaki historia yake lafudhi yake au hata kazi aliyokuwa anafanya ila Mungu keshampa kibali cha kuwa hapo’
Hata huyo Askari ukute alimpigia kura Hillary ila anajikuta akitii mamlaka ya Melania, Kiongozi anaweza akatoka sehemu chakavu isiyo na tumaini, chini, mwisho kabisa… Kumbuka hata Bwana Yesu alizaliwa katika zizi la ng’ombe."
Mungu anaweza kumuinua mtu usiyemtarajia na kumfanya mtawala wako, Mungu anaweza kukuinua wewe usiyejidhania na kukuweka mahali pa juu, mipango yake si kama yetu, usidharau mtu yeyote na muhimu usijidharau, njia zake si kama zetu #TujifunzeKitu #BeHumble
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive