Leo ndio siku ambapo rasmi raisi Barack Obama anaondoka ikulu,Donald
Trump anaenda White House baada ya kuchaguliwa na wananchi wa
Marekani.Maraisi wote hawa wana upenzi katika michezo huku Obama akiwa
katika kikapu lakini kama hujui nikujuze kuwa Trump ni kati ya watu
waliowahi kuwekeza pesa nyingi katika michezo haswa wa mieleka.
Obama anaondoka Marekani akiwa raisi ambae alikuwa kipenzi cha watu
wengi duniani.Obama alikuwa mpenda michezo na kama ilivyo ada ya
Wamarekani mchezo kwa kikapu ndio mchezo wao mkuu.Akiwa White House
Obama alipata nafasi kuzialika timu mbali mbali za kikapu.
Mwaka 2012 Barack Obama alikutana na timu ya kikapu ya Dallas
Mavericks,abapo katika mualiko huo mchezaji wa Dallas Dalonte West
aliishia getini.West alishindwa kuingia kuonana na Obama kutokana na
kuwa na rekodi ya kumiliki silaha kinyume cha sheria.
Lakini mwaka jana pia mwezi wa 11 mabingwa wa ligi ya kikapu ya NBA
Cleveland Cavariels wakiongozwa na Lebron James walienda White House kwa
mwaliko maalumu kukutana na Barack Obama.Baada ya kuwafunga wapinzani
wao Golden State Warriors timu hiyo ilifunga safari hadi kwa Obama hiyo
ikiwa siku mbili kabla ya uchaguzi wa Marekani.
Lakini Golden State Warriors pamoja na kufungwa na Cavs ila wao
walishatangulia ikulu kabla yao kwani April mwaka jana wakiwa na Steph
Curry walienda hadi ikulu kukutana na raisi Obama.
Obama hakuwa anajua kuhusu kikapu tu hata soka pia yumo,ambapo mwanae
Sasha ni shabiki mkubwa wa Lioneil Messi.March mwaka 2016 mchezaji wa
Argentina Lioneil Messi alisema anatamani kukutana na raisi Barack
Obama.Messi aliongea haya baada ya mtoto wa Obama aitwaye Sasha
kumuambia baba yake kwamba anatamani kumuona Messi.Katika ziara yake
nchini Argentina Obama aliwaeleza watu kuhusu tamanio hilo la mtoto
wake.
Obama hakuanza kumjua Messi hapi kwani mwaka 2011 wakati akipewa jezi
namba 10 kutoka timu ya Colorado Rapids Obama aliwatania Colarado na
kusema “nashukuru munajua kuwa namba 10 ndio kiongozi kwahiyo mimi na
messi ni viongozi”
Lakini katika utawala wa Obama Manchester United pia walitembelea
White House.Hiyo ilikuwa mwaka 2011 lakini kutokana na majukumu Obama
alishindwa kukutana na timu hiyo.
Sasa anakuja Donald Trump mfanyabiashara mkubwa ambae ameshawahi
kuinvest pesa kubwa sana katika mieleka.Kuanzia leo Trump anaingia
madarakani baada ya kuchaguliwa na wananchi wa taifa hilo
kuliongoza.Pengine hujui au umesahau kuhusu Trump na WWE(World Wrestling
Entertiment)basi leo tunakujuza na kukumbusha.
Mwaka 2007 katika plaza ya Trump iitwayo Donald Trump Plaza
iliyokohuko New Jersey iliandaa mpambano wa Wrestlmenia IV na
Wrestlmenia V na plaza hiyo kuingia katika historia ya shoo hiyo kwa
kuiandaa mara mbili katika miaka miwili mfululizo.
Katika mwaka huo mwezi January Trump alimtibua mwenyekiti wa WWE
MR.McMahons katika usiku ulioiywa “Night Of Apreciation”.Trump alirusha
dola elfu kumi katika uwanja huo kwa mashabiki.Mcmahon hakukubali
aliitisha mpambano ulioitwa “Battle Of Billionaires” katika pambano hilo
kila bilionea alichagua mpiganaji wake na mpiganaji wako akishindwa
unanyolewa nywele.Pambano hili liliisha kwa mpiganaji wa Trump aitwae
Bob Rashley kudshinda dhidi ya Umaga wa Mcmahon na hivyo Trump kumnyoa
Mcmahon nywele mbele za watu.
Trump ana historia kubwa na mieleka,mwaka 2009 yeye ndiye alikua
akiandaa usiku wa mieleka ujulikanao kama Monday night raw.Trump
anaingia madarakani sasa sijui kama atauacha moja kwa moja uhusiano wake
na mieleka.Lakini pia haitakuwa ajabu kuwaona kina John Cena na
Undertaker kuhudhuria White house kwa wingi.
0 comments:
Post a Comment