Rais mteule wa Marekani Donald Trump mwenye umri wa miaka 70, anaapishwa saa chache zijazo Washington DC. Marekani kuwa Rais wa 45 wa Marekani akichukua kiti kinachoachwa na Barack Obama
Miongoni mwa wataohudhuria kuapishwa
huko ni pamoja na Waziri wa zamani wa maliasili na utalii Tanzania
Lazaro Nyalandu ambaye tayari ameshawasili Washington DC saa kadhaa
zilizopita.
Nyalandu ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Singida Kaskazini ameviambia vyombo vya habari kuwa‘Nimewasili Washington DC mapema leo na kushiriki mwaliko wa Maseneta Chuck Grassley na Joni Ernst wakiwa na wajumbe wa Baraza la wawakilishi toka Jimbo la Iowa, wakiongozwa na Steve King‘
‘Jimbo la Iowa ni mahali nilisoma chuo miaka ya nyuma, tukio la mchana huu limefanyika hapa US Capitol Hill, asubuhi kesho nitashiriki hafla ya kuapishwa Donald J Trump kwa mwaliko wa kamati ya maandalizi ya Baraza la Congress na nitatarajia kurudi nyumbani kuendelea na vikao vya Bunge’ – Nyalandu
0 comments:
Post a Comment