Yahya Jammeh ambaye amekua madarakani na kuingoza Gambia kama Rais kwa miaka 22 hatimae amekubali kuachia madaraka hayo na sasa Adama Barrow aliyetangazwa mshindi kwenye uchaguzi mkuu ndio anatarajiwa kuchukua nafasi.
Kupitia Television ya taifa, Yahya ametangaza kuachia madaraka ambapo AlJAZEERA wameripoti kwamba taarifa kutoka IKULU
zilisema baada ya kuachia madaraka alitarajiwa kuondoka kwenye nchi
hiyo ndani ya siku 3 ila media nyingine zinasema amepewa saa tu za
kuondoka.
TV ya habari Nigeria imesema ECOWAS
walimpa hadi saa sita mchana kuondoka lakini mwenyewe akaomba muda huo
usogezwe hadi saa kumi jioni na imeripotiwa atakwenda kuishi Guinea.
Barrow aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter na kusema ‘Yahya Jammeh amekubali kuachia madaraka na anatarajiwa kuondoka kwenye nchi ya Gambia leo’
0 comments:
Post a Comment