Msanii wa muziki wa bongo fleva Ommy
Dimpoz ambaye bado anafanya vyema na wimbo wake 'Kajiandae' amefunguka
na kusema hajapangishiwa nyumba Mbezi na jimama kama ambavyo inadaiwa na
kudai kuwa kwa sasa yeye anaishi Mikocheni.
Ommy Dimpozi akiongea na EATV alisema
hana nyumba ambayo amepangisha wala hajapangishiwa nyumba ila kwa sasa
anafanya ujenzi katika viwanja vyake viwili Mbezi pamoja na Kigamboni.
"Unajua binadamu wanaweza kuongea hiki na hiki lakini ukweli ni kwamba mimi naishi Mikocheni kwenye apartment hivyo siishi Mbezi, ila Mbezi kuna sehemu nina site yangu ambayo najenga na site nyingine ipo Kigamboni.
Kwa hiyo sina nyumba ambayo nimepangisha
au nimepangishiwa kwa hiyo hizo stori sijui bimkubwa sijui nini siyo
kweli, mimi mambo yatakapokuwa tayari nitamuweka wazi mtu wangu ila demu
wangu si Mzungu ni Mchina" alisema Ommy Dimpoz.
0 comments:
Post a Comment