UONGOZI wa Azam FC hivi karibuni unatarajia kukipeleka kikosi chao nchini Rwanda alipo kiungo Haruna Niyonzima kwa ajili ya kwenda kucheza mechi za kirafiki baada ya kupata mwaliko maalumu kutoka kwa timu ya Rayon Sports ya nchini humo.
Kikosi hicho kimepata mwaliko huo wa kwenda Rwanda ikiwa ni siku
chache baada ya kuanza kambi yake ya kujiandaa na msimu ujao ambapo
kikosi hicho kitaondoka hapa nchini Julai 6 mwaka huu.
Msemaji wa Azam Jaffar Idd amekiambia moja kati ya vyombo vya habari hapa nchini kuwa wamepata mwaliko huo kutoka kwa Wanyarwanda hao anapotokea Niyonzima wa kwenda kucheza mechi za kirafiki kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi.
“Tayari sisi tumeanza kambi yetu kwa ajili ya msimu ujao wa ligi
ambapo tuliingia kambini juzi Jumatano kwa baadhi ya nyota wetu waliopo
hapa nchini kuja lakini bado wengine watawasili hivi karibuni.
“Lakini Julai 6 tutaenda Rwanda ambapo tumepata mwaliko kutoka kwa timu ya Rayon Sports ya
huko kwenda kucheza mechi za kirafiki na tumepanga kutumia faida ya
mechi hizo kama sehemu ya maandalizi yetu ya msimu ujao wa ligi kuu.”
alisema Jaffar.
0 comments:
Post a Comment